Majonzi!
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki amepata
pigo kubwa la kufiwa na mkewe, Shuea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya kuugua
kwa muda mrefu.
Aliyekuwa mke wa Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa
Kizigo’, Ali Choki, marehemu Shuea Hamis ‘Mama Shuu’. Akizungumza na
Ijumaa Wikienda kwa masikitiko, Choki alisema kwamba mke wake ameugua
kwa muda wa miezi tisa akisumbuliwa na tatizo la mguu.
Alisema kwamba katika jitihada za matibabu, mkewe huyo alitibiwa
nchini India ikashindikana, akarudishwa nyumbani mpaka mauti yalipomfika
usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
“Kweli alikuwa akipata mateso makubwa kwani alikuwa hatembei analala
tu ndani hivyo kutoa nafasi kwa magonjwa mengine kumshambulia.
“Ukweli nimeumia kwani alikuwa ni mshauri wangu mkuu na ndiye alikuwa kila kitu kwangu.
“Alikuwa akinisapoti sana kwenye kazi yangu ya muziki lakini ndiyo
hivyo Mungu amempenda zaidi sina la kufanya,” alisema Choki kwa majonzi.
Ali Choki akiwa kwenye picha ya pamoja na mkewe enzi za uhai wake.
Choki alisema mipango ya mazishi ilifanyika nyumbani kwake Tuangoma,
Kigamboni jijini Dar na mazishi ya mkewe yalitarajiwa kufanyika jana
Jumapili, saa 10:00 jioni katika Makaburi ya Maduka-Mawili, Chang’ombe,
Dar.
Mama Shuu alikuwa mdau mkubwa wa muziki wa dansi Bongo hivyo ni pigo
kubwa kwa tasnia hiyo. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Amina.
EmoticonEmoticon