UZURI NA UBAYA SEHEMU YA TATU



MSIMULIAJI:SAIMENI MGALULA


Endelea basi wale wafuasi wakatoka kwa kasi ya hajabu na kwenda maeneo yale lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kumuona Yule bibi alishakuwa ameshatoweka na kuingia mitini wao walicho amua ni kurudi kwa mfalme na maneno tu kuwa sisi atuja mkuta .

Mfalme oga alishajua kuwa Yule bibi ndo aliyenipa lana mimi ikabidi atafutwe mganga wa kienyeji iliaweze kumtibu Yule mfalme oga pamoja na hayo mganga hakuwa mbali alikuwa katika kijiji kile kile cha Swai alikuwa akiwasaidia watu kwa tiba za asili. Na alikuwaanaitwa kalulunge

Basi ilikuwa ni siku ya juma tatu mishale ya saa mbili asubuhi katika kijiji cha swai hali ya hewa ilikuwa mbaya sana kutokana na mizimu kuchukia jinsi mfalme oga alivyokuwa anawanyanyasa wananchi pale kijijini  ndipo mganga kalulunge aliwasili kwa mfalme oga alikutana na mlinzi akajieleza shida yake ndipo akapewa ruksa akaingia ndani .

Alipoingia ndani bila ya kuchelewa kutokana na mfalme alivyokuwa kama sokwe na kuchachawa kwake ilibidi amfariji kwa kumwambia kuwa utapona ilia endapo tutamkuta binti bikira ambaye haja wahi kufanyiwa kitu chochote katika mwili wake .

Baada ya mazungumzo hayo mfalme aliwahamuru wafuasi wake kwenda kukamata mabinti mpaka apatikane bikira kwa bahati nzuri katika mabinti walioshikwa mia moja walimpata bikira wakamuamuru aingie kwenye chumba cha mfalme iliwafanye vitu na kusababisha kupona kwa babadiliko yake ya kimaumbile.

Kitu walichomfanyia Yule bikira ni kumtoa kafara ili damu yake aogee mfalme oga na akisha oga atapona ndivyoalivyosema mganga kalulunge sasa je mra baada ya kufanya hivyo je atapona kwa mbinu alivo mpa mganga kalulunge.

Mara baada ya kafara mfalme alipelekwa bafuni na kuoga baada ya kuoga ziledawa za mganga kalulunge ziligonga ukichanganya na lana na dhambi alizofanya tena za kumtoa kafara binti bikira ambaye hana hatia yeyote kisa mfalme oga .
Mfalme oga kwa hasira tena na kuona hali haija badilika aliamuru wafuasi wake tena  kwa mara nyingine waende wakamate wamama wote iliakawakague kama yupo Yule bibi aliye mpa lana kutokana na unyanyasaji wake wa kumnyima chakula tu.

Wafuasi wake walichukuwa gari kubwa kama wanazo bebea wafungwa na kwenda kuwachukuwa wamama wote  na kuwaingiza uwanjani kwa mfalme lakini cha hajabu na chakusikitisha kwa wale wamama alikuwemo mama yake Swaumu chacha ambaye anamwanaye anaye itwa swaumu chacha anaye fatiliwa na Cash money.

Mfalme baada ya kuwakagua hakuweza kumpata alichokisema ni kuwaachia huru wamama wote ila isipokuwa mama yake Swaumu ambaye alichukuliwa na kuingizwa kwenye gereza dogo palepale kwa mfalme mpaka atakapo Yule bibi maskini mama wawatu hana hatakosa lolote lile amefungwa jamani mmmmm kweli wanaokwenda jera sio wote wanahatia.

Sasa tukaona Swaumu anajitoa kwenda kwa mfalme ili afungwe yeye mama yake achiwe je mfalme atakubali na akikubali Yule cash money atafanya nini ataenda kumtoa au atamuacha

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng