·
MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.
·
MTU MMOJA MKAZI WA AIRPORT JIJINI MBEYA
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI AKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA SHORT GUN NA
RISASI SABA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIWA
WATU WAWILI WAKIWA NA BHANGI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU
WATATU WAKIWA NA POMBE YA MOSHI LITA 30.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTEMBEA KWA
MIGUU ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ATUSUNGUKILE
MAHENGE (23) MKAZI WA UYOLE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA
GARI ISIYOFAHAMIKA ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI YAKE.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.10.2014
MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI HUKO
NANE NANE DARAJANI, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA
JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] KUZITOA KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA
PILI:
MTU MMOJA AITWAYE EMANUEL MWAKEJA (27) MKAZI WA PAMBOGO – AIRPORT ALIKUTWA AKIWA NA
SILAHA BUNDUKI MOJA AINA YA SHORT GUN IKIWA NA RISASI SABA [07] NYUMBANI KWAKE BAADA YA KUPEKULIWA.
MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 26.10.2014 MAJIRA YA SAA 18:40 JIONI HUKO PAMBOGO, KATA YA
IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, MNAMO TAREHE 26.10.2014 MAJIRA YA SAA 17:45 HUKO MAENEO YA UWANJA WA SOKOINE,
KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA MTU MMOJA AITWAYE ALFONCE MWAKASEGE (38) MKAZI WA
MAKUNGURU ALIGUNDUA KUIBWA KWA PIKIPIKI YAKE YENYE NAMBA ZA USAJILI T.683 BDM AINA YA KINGLION NA
KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WAWILI AMBAO NI 1.
JOSEPH KIGULU (24) MKAZI WA AIRPORT NA 2.
JUMA NELSON (31) MKAZI WA IYELA.
WATUHUMIWA HAO BAADA YA KUKAMATWA NA
KUHOJIWA WALIDAI KUWA PIKIPIKI HIYO IPO NYUMBANI KWA EMANUEL MWAKEJA NA WALIPOKWENDA WALIIKUTA NJE NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA. MTUHUMIWA HUYO
ALIPEKULIWA NYUMBANI KWAKE NA NDIPO ALIKUTWA NA SILAHA BUNDUKI MOJA AINA YA
SHORT GUN NA RISASI SABA IKIWA IMEWEKWA CHINI YA GODORO CHUMBANI KWAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA
AITWAYE ALBERT LAISON (31) MKAZI WA
LUALAJE ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI NUSU DEBE.
MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 25.10.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI
CHA KABUTA, KIJIJI CHA LUALAJE, KATA YA LUALAJE, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MAENEO HAYO. MTUHUMIWA NI MUUZAJI
WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
AIDHA,
KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MASHAKA ALLY (19) MKAZI WA CHIMALA
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI DEBE MOJA NA NUSU.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 25.10.2014
MAJIRA YA SAA 13:20 MCHANA HUKO
CHECK POINT – INYALA, KATA YA INYALA, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBALIZI,
MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUTWA NA BHANGI HIYO ALIYOKUWA AMEIWEKA KWENYE MFUKO WA SULPHATE AKIWA ANAISAFIRISHA
KUTOKA CHIMALA KWENDA MBEYA MJINI KWA MAUZO. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI
WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA TATU, WATU WATU
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. JULIUS
CHUWALO (56) 2. EDINA CHARLES (44)
NA 3. EVA MSOKWA (40) WOTE WAKAZI WA
MLOWO WAKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA
LITA 30 NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO HARAMU.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 25.10.2014 MAJIRA
YA SAA 08:00 KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MLOWO, KATA YA
MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI
WA POMBE HIYO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
AIDHA, ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU AU MTANDAO
WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA BIDHAA HARAMU ILI WAKAMATWE
NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon