Jeshi la Polisi mkoani Pwani
limefanikiwa kumkamata Michael William maarufu (Michael dada), mkazi wa
Kiluvya, wilayani Kisarawe anayetuhumiwa kuhusika na matukio ya ubakaji
wa vikongwe mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa
Pwani Ulrich Matei alisema jeshi hilo lilikuwa likimsaka mtuhumiwa huyo
kwa kipindi kirefu kutokana na kudaiwa kutenda makosa mbalimbali ya
ubakaji wa vikongwe na wanawake na kutokomea kusikojulikana.
Alisema, William alitiwa mbaroni juzi baada ya kudaiwa kuhusika
katika tukio la wizi wa mifugo lililotokea wiki mbili zilizopita huko
Kiluvya.
Pia kamanda Matei alisema, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuhusika
katika matukio ya ubakaji zaidi ya 10 ambapo kabla ya kufanya vitendo
hivyo alikuwa akiwatishia wahusika kwa mapanga.
“Huyu kijana anayejiita Michael dada ni maarufu kwa matukio ya
ubakaji na alilisumbua jeshi letu mara kadhaa kwa kunasua mitego
aliyowekewa leo tumelazimika kumleta mbele yenu waandishi ili mumuone ni
mdogo lakini ametusumbua sana,” alisema.
William alikiri mbele ya waandishi wa habari kuwa miaka ya hivi
karibuni aliwahi kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha kosa ambalo
lilimsababishia kuhukumiwa miaka 30 jela.
Matei alisema kabla kifungo hicho hakijamalizika mwaka 2011 na
2012, William alikata rufaa na kutolewa ili kuendelea na taratibu
nyingine na tangu hapo hakuonekana hadi polisi walipofanikiwa kumkamata
kwa kosa la wizi wa mifugo.
Hata hivyo William alikana kuhusika na tuhuma zinazomkabili na
kudai yeye sio Michael dada kama anavyoitwa bali ni Michael William na
tuhuma za ubakaji ni za kusingiziwa
EmoticonEmoticon