·
DEREVA WA GARI LA ABIRIA AFARIKI DUNIA BAADA YA MAGARI MAWILI KUGONGANA
ENEO LA MWISHO WA WAYA.
·
MTU MMOJA MKAZI WA MKWAJUNI WILAYA YA CHUNYA
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI.
·
MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.]
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NA KETE 12 ZA BHANGI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NA POMBE YA MOSHI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
DEREVA MMOJA KATI
YA WAWILI AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME,
UMRI KATI YA MIAKA 25 - 30 AMEFARIKI
DUNIA BAADA YA MAGARI YA ABIRIA WALIYOKUWA WAKIENDESHA YENYE NAMBA ZA USAJILI T.473 CNT AINA YA TOYOTA HIACE NA GARI T.135 AJF AINA YA TOYOTA HIACE
KUGONGANA USO KWA USO ENEO LA MWISHO WA WAYA.
AJALI HIYO
IMETOKEA MNAMO TAREHE 22.10.2014
MAJIRA YA SAA 22:20 USIKU HUKO
MAENEO YA MWISHO WA WAYA, KATA YA IYUNGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA.
AIDHA, WATU
WATATU WALIJERUHIWA KATIKA AJALI HIYO AMBAO NI 1. LAMECK LIMO 2. ANGOLISYE
MWAKALOBO NA 3. JOYCE ASAJILE
AMBAO WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU.
CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA MKAZI WA MKWAJUNI WILAYA YA CHUNYA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PRISCA SINKALA
(31) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI
[GONGO] UJAZO WA LITA 05.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.10.2014
MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MAJENGO, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU
ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
AITWAYE ISAYA DARON (27) MKAZI WA
SOWETO AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU AINA YA BOSS PAKETI 30.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.10.2014
MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO
SOWETO, KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI
MUUZAJI WA POMBE HIZO.
KATIKA MSAKO WA TATU, MTU MMOJA MKAZI
WA AIRPORT JIJINI MBEYA AITWAYE SALEHE
SEKILE (32) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA KETE 12 ZA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAMU 60.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE
22.10.2014 MAJIRA YA SAA 17:30 JIONI
HUKO MAENEO YA FOREST MPYA, KATA YA FOREST, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA
WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUTWA NA KETE HIZO BAADA YA KUPEKULIWA KWENYE MIFUKO
YAKE YA SURUALI. AIDHA, MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI HIYO.
KATIKA
MSAKO WA NNE, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI
WAKAZI WA MANGA JIJINI MBEYA AMBAO NI 1. TERESIA MWAISAKILE (31) NA 2. ELIZABETH LONDELE (29) WAKIWA NA
POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 01.
WATUHUMIWA KWA
PAMOJA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIENDESHWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
MNAMO TAREHE 22.10.2014 MAJIRA YA SAA 13:30 MCHANA HUKO MAENEO YA MANGA,
KATA YA MANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI
WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA/POMBE YA MOSHI PAMOJA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA, ANATOA WITO KWA
WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UINGIZAJI/USAMBAZAJI NA
UUZAJI WA POMBE KALI NA POMBE YA MOSHI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon