Mtu
mmoja amefariki Mkoani Iringa baada ya lori lililobeba mafuta kupinduka
na kuteketea kwa moto kisha kusababisha majeruhi kwa mmoja
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP. Ramadhani
Mungi amemtaja marehemu kuwa ni Tony Shilla mkazi wa mkoani Mbeya ambaye
amefariki papo hapo kwa ajali ya moto huo.
Kamanda
Mungi ameongeza kuwa Brayton Mwambongika umri wa miaka 34 dereva wa
gari hilo lenye namba za usajili T 198 CZS aina ya Scania amejeruhiwa
ambapo amelazwa katika hospitali ya rufaa mkoani Iringa akiendelea na
matibabu zaidi.
Hata
hivyo Kamanda Mungia meongeza kuwa ajari imetokea maeneo ya Igeme,
tarafa ya Mahenge, wilayani Kilolo, mkoani Iringa na jeshi la polisi
Mkoani Iringa linaendelea na kufanya uchunguzi zaidi wa kubaini chanzo
cha ajali hiyo
EmoticonEmoticon