WATU wawili wamefariki dunia katika ajali mbaya ya pick up kugongana na lori katika eneo la Kibwabwa barabara kuu ya Iringa - Mbeya usiku wa kuamkia leo
Kwa mujibu wa mashuhuda ajali hiyo imesababishwa na dereva wa gari dogo kuhama upande wake na kulifuata lori hilo kampuni ya Pro-Trans Ltd ya jijini Dar es Salaam ambalo lilikuwa likitokea barabara ya Mbeya kuja Iringa na gari hilo dogo lilikuwa likitokea Iringa mjini.
Akielezea tukio hilo mmoja kati ya mashuhuda John Sanga alisema kuwa wakati ajali hiyo ikitokea alikuwa katika kituo cha Mafuta kilichopo eneo hilo na kushuhudia jinsi ambavyo dereva wa pick up hiyo akilifuata lori hilo kabla ya kutokea ajali hiyo mbaya .
Hata hivyo alisema dereva wa gari hilo dogo alionyesha kumfuata dereva wa lori ambapo dereva huyo ya lori alionyesha jitihada za kumkwepa bila mafanikio .
Alisema katika ajali hiyo dereva alikufa papo hapo huku abiria wake alikimbizwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na kufariki wakati akipatiwa matibabu
SOURCE : FRANCIS GODWIN
|
EmoticonEmoticon