TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14.03.2014.

  


JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WAKIWA NA BHANGI.


JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WAKIWA NA BHANGI.

KATIKA MSAKO ULIOENDESHWA NA JESHI LA POLISI JANA MAJIRA YA SAA 13:45 MCHANA WATUHUMIWA WAWILI WALIKAMATWA AMBAO NI 1. ISAYA AMBOKILE (22 MKAZI WA KAGERA NA 2. TEGEMEO MWINUKA (23) MKAZI WA ILEMI WAKIWA NA BHANGI KETE 03 SAWA NA UZITO WA GRAM 15. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MTAA WA KAGERA, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA.

AIDHA KATIKA MSAKO MWINGINE ULIOFANYIKA MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA MTAA WA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA   MKOA WA MBEYA MTUHUMIWA JASON PAUL (26) MKAZI WA IYELA II ALIKAMATWA AKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO MOJA IKIWA KWENYE MFUKO MWEUSI WA RAMBO. MTUHUMIWA ALIKUTWA NA BHANGI HIYO BAADA YA KUPEKULIWA.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA MAHAKAMANI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU/MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »