TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 31.03.2014.
WATU WASIOFAHAMIKA WAFANYA UHARIBIFU WA MALI PAMOJA NA KUUA MIFUGO
WILAYA YA MOMBA.
WATU WASIOFAHAMIKA WAFANYA
UHARIBIFU WA MALI PAMOJA NA KUUA MIFUGO [MBUZI] WAPATAO 15 KWA KUWAKATA KWA
MAPANGA MALI YA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA USOKE WILAYA YA MOMBA ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA STANSLAUS SIMWICHE (50).
KATIKA TUKIO HILO WATU HAO WALIFANYA PIA UHARIBIFU KWA KUBOMOA NYUMBA YAKE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
30.03.2014 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA
KIJIJI CHA USOKE, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA
TUKIO HILO NI IMANI ZA KISHIRIKINA BAADA YA MWENYEKITI HUYO KUTUHUMIWA KUMROGA
MAREHEMU FRANK ABEID ALIYEFARIKI
MNAMO TAREHE 27.03.2014 HUKO TUSULU.
THAMANI HALISI YA MALI ILIYOHARIBIKA NI SHILINGI 5,654,000/=. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALE WOTE WALIOHUSIKA NA TUKIO
HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA
KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII NA BADALA YAKE WATATUE MIGOGORO YAO KWA
NJIA YA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO.
Signed
by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon