TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 16.10.2014.
·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA
WAKISAFIRIA KUPINDUKA WILAYANI RUNGWE.
·
MTOTO WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUTUMBUKIA KWENYE NDOO YA MAJI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA MKAZI WA IYUNGA JIJINI MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO].
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA LUSEKERO AMBILIKILE (36), TINGO NA MKAZI WA BULYAGA –
TUKUYU ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.920 BSW AINA YA FUSO TIPPER
LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE SETH
HAMAD KUPINDUKA ENEO LA KATUMBA WILAYA YA RUNGWE.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 16.10.2014 MAJIRA YA SAA
19:40 JIONI HUKO MAENEO YA KATUMBA, KATA YA BAGAMOYO, TARAFA YA TUKUYU,
WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU. CHANZO CHA
AJALI NI MWENDO KASI.
DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA KULITELEKEZA
GARI ENEO LA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANA – RUNGWE.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 03 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JORIN WILLIAD [JINSI YA KIKE] MKAZI WA GHANA JIJINI MBEYA AMEFARIKI
DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE NDOO YA MAJI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 16.10.2014 MAJIRA YA SAA
09:45 ASUBUHI HUKO MAENEO YA
GHANA MASHARIKI, KATA YA GHANA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, CHANZO CHA KIFO HICHO NI BAADA YA MTOTO HUYO KUTAKA KUTOA KIATU
CHAKE KILICHOKUWA NDANI YA NDOO NA KATIKA HARAKA HIZO NDIPO ALITUMBUKIA KWENYE
NDOO HIYO ILIYOKUWA NA MAJI NA KUFARIKI DUNIA.
MWILI WA NAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA
KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWEKA UANGALIZI WA
KUTOSHA KWA WATOTO WADOGO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA,
ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA, KUFUKIA MASHIMO KWANI NI HATARI KWA
WATOTO WADOGO.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
MKAZI WA IYUNGA JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GRACE MBUILONGO (48) AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO
WA LITA 10.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 16.10.2014 MAJIRA YA SAA
13:00 MCHANA HUKO MAENEO YA IYUNGA, KATA NA TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA
WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO KATIKA MAENEO HAYO. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA
MTUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon