Wafanyakazi wa Zahanati ya kivukoni mkoani Morogoro wazalisha na kushona wagonjwa kwa tochi.







Photo: Wafanyakazi wa Zahanati ya kivukoni mkoani Morogoro wazalisha na kushona wagonjwa kwa tochi.->http://bit.ly/1yh916e






Wafanyakazi wa Zahanati ya kivukoni, kata ya Minepa,tarafa ya Lupiro wilayani Ulanga mkoani Morogoro, wamekuwa wakitumia tochi kushona wagonjwa au kuzalisha wajawazito wanaofika kwa dharura nyakati za usiku, kutokana na kukosekana umeme au nishati nyingine mbadala ya kuwawezesha kupata mwanga katika zahanati hiyo.
Wakizungumza na ITV katika zahanati hiyo, inayohudumia takribani wagonjwa 30 kwa siku, wafanyakazi hao wamesema iwapo serikali itatilia mkazo changamoto hiyo kwa haraka, kuna uwezekano mkubwa wa kusaidia kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto, sambamba na kuboresha zaidi utoaji wa huduma, huku wananchi wa kivukoni wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara, wamesema pamoja na kujisajili kwenye mifuko ya afya ya jamii, bado huduma zinazotolewa katika  zahanati hiyo haitoshelezi, jambo linalowazimu kufuata huduma hizo makao makuu ya tarafa ambako ni mbali.
 
Aidha wananchi wameeleza kushangazwa kuona nyumba za watu zilizojirani na zahanati hiyo zinafungiwa umeme, huku eneo hilo muhimu kwa jamii likikosa huduma hiyo, ambapo mbunge wa jimbo la Ulanga magharibi Dk Haji Mponda, amesema tayari serikali imeona changamoto hiyo na kutenga kiasi cha shilingi milioni saba kufikisha umeme katika zahanati hiyo na kinachokwamisha hivi sasa ni utaratibu wa malipo ya serikali.
Previous
Next Post »