![Photo: Wazee waliopigana vita vya pili vya dunia walalamikia kutolipwa pesa zao.kwa taarifa zaidi bofya->bit.ly/1kuwtf5](https://fbcdn-sphotos-b-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xfp1/t1.0-9/p526x296/10550835_588408054603506_3118396295173435572_n.png)
Wazee waliopigana vita vya pili vya dunia pamoja na warithi wa madai yao wamelalamikia kutolipwa fedha zao walizodai zilitolewa na serikali ya uingereza na kulalamikia kutokabidhiwa jengo lao walilokabidhiwa na serikali hiyo mwaka 1947 huku halmashauri ya wilaya ya Songea ikidai ni mali yao.
Ni kauli mbiu ya wazee waliopigana vita ya pili ya dunia pamoja na warithi wa madai yao katika mkoa wa Ruvuma wakiwawakilisha wenzao wao mikoa ya Mtwara na Lindi wanaodai fedha zao na jengo lao walilokabidhiwa na mwingereza mwaka 1947 huku halmashauri ya wilaya ya Songea ikidai wamerithishwa jengo hilo mwaka 1994.
Katika jengo hilo linalogombewa na pande hizo mbili lina ukumbi ambako halmashauri hufanyia vikao vyao na ndiko ziliko ofisi za idara ya elimu ya halmashauri ya wilaya ya Songea.
Katika sakata hilo ITV imefanikiwa kuzungumza na wazee wawili waliosalia waliopigana vita ya pili ya dunia huku wengine wakiwa ni warithi wa madai ya wapiganaji wa vita hivyo ambao ni Francis Soko mwenye umri wa miaka 96 na Mussa Kisonga mwenye umri wa miaka 9o.
EmoticonEmoticon