Mtu mmoja auawa kikatili kisha mwili wake kuchomwa moto Morogoro.

Mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja ameuwawa kikatili kisha mwili wake kuchomwa moto na watu wasiofahamika  katika eno la mkundi manispa a ya  Morogoro.
Kwa mujibu wa wananchi walishuhudia tukio hilo  wamesema   wameshuhudia kundi la madereva wa pikipiki wakimshusha mtu huyo kisha kumwagia mafuta ya taa na kumchoma moto ambapo wameomba jeshi la polisi kufuatilia tukio hilo walohusika wachukuliwe hatua.
 
Wananchi wakazi wakata ya mkundi  wamesema hilo sio tukio la kwanza kutoke kwa watu kuuwawa na kisha kuchomwa moto na kuomba vyomba vya sheria kufanya kazi zake kwani huenda matukio hayo yanatokana na watu kuchoshwa na baadhi ya matukio ya wizi ambayo watuhumiwa huachiwa huru na vyombo vya sheria pasipo kuchukuiwa hatua.
 
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kw atukio hilo na limefika katika eno la tukio.
Previous
Next Post »