MWIZI WA BODABODA AUAWA KWA KUCHOMWA MOTO MBAGALA


Photo: Siku za mwizi malizien ndgu
kijana ambae anahisiwa ni mwiz wa Boda boda akiwa ameuawa kwa kuchomwa na moto na raia wenye hasira kali maeneo ya Mbagala charambe

Photo: Habr ndg huyu ndye mwizi wa bodaboda raia walivyo fanya kaz yao bada ya kukamata 

huu ni muendelezo wa uchukuaji sheria mikononi kwani mapema mwaka huu Madereva wa bodaboda walichoma Daladala kwa madai ya kugonga mtu ambapo madereva hao walilifukuza gari hilo mpaka eneo hilo la charambe kwa Mbiku  ambapo dereva wa gari hilo alishindwa kulidhibiti akalidondosha ndipo maderva hao  wakalimwagia petroli gali hilo na kuliwasha na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali
lakini uchunguzi wa blog pendwa hii unasema huyo mwananchi ambae alikua amegongwa na hiace hiyo aliruhusiwa siku hiyo hiyo Hospitali na hakua amepata maumivu makubwa

kutoka kwenye Meza ya Dar24habari.com

Tunawasihi wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi kwani tabia hii imetufanya tupoteze watu wengi bila hatia ngazi za sheria zipo kama mnamshuku ni mwizi apelekwe kwenye vyombo vya dola ambavyo vyenyewe vitachunguza na kujua ukweli wake na vitatoa adhabu kulingana na kosa kitendo cha kuwaua washukiwa ni uvunjifu wa sheria na pia ww ulieuwa ndio unakua umetenda kosa kubwa kuliko huyo mwizi uliemuua kwakua mwizi alitaka kuiba Bodaboda wewe umeua nani mwenye kosa kubwa? wakati bado hata mioyo ya watanzania haijapoa tukimkumbuka mwanafunzi wa Sheria Mbeya aliyeuwawa kikatili kwa kuchomwa moto kwa kuhisiwa mwizi kumbe alienda kutafuta chakula  je hali hii ya kuwaua watu wasio na hatia itaisha lini??? Mwananchi chukua hatua waripoti watu wenye tabia hii ili umponye nduguyo je unajuaje kesho akahisiwa,Mumeo,Mkeo,kaka yako au mdogo wako??
Previous
Next Post »