HUU NI UJUMBE ALIOUANDIKA MH.MARK MWANDOSYA KATIKA UKURASA WAKE WA FACEBOOK



Miaka mitatu iliyopita ilitangazwa na 'marafiki' zangu, mara tatu, kwamba Profesa Mwandosya amefariki.Baada ya hilo kutotimia wakasema nina miezi mitatu tu ya kuishi! Niliwashukuru kwani hakika walikuwa wananitakia maisha marefu.Leo ninaposherehekea siku ya kuzaliwa,namshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha nikitambua vilivyo majukumu yanayoendana na bahati hiyo.Nawashukuru familia,ndugu,marafiki na watanzania wenzangu wengi mlionitakia heri na afya njema.Asante sana.
Like ·  ·  · 2061703 ·
Previous
Next Post »