MKUTANO WA KAMANDAWA POLISI MKOA WA MBEYA NA WAANDISHI WA HABARI “PRESS CONFERENCE” KUHUSIANA NA HALI YA UHALIFU KWA KIPINDI CHA NUSU MWAKA JAN – JUNI - 2014.





Ø  JUMLA YA MAKOSA YOTE MAKUBWA NA MADOGO YA JINAI NA USALAMA BARABARANI.

Ø  MAKOSA KERO KWA JAMII.

Ø  MAKOSA YATOKANAYO NA JITIHADA ZA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU NA WANANCHI.

Ø  MAFANIKIO

Ø  CHANGAMOTO.


Ø  WITO WA KAMANDA.

HALI YA UHALIFU.

KWA UJUMLA HALI YA UHALIFU MKOA WA MBEYA KWA KIPINDI CHA JAN- JUNI, 2014 ILIKUWA SHWARI. AIDHA MAKOSA MBALIMBALI YALIRIPOTIWA KUTOKEA IKIWA NI PAMOJA NA MAUAJI, UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA/NGUVU, KUBAKA, UVUNJAJI, WIZI WA MIFUGO, PIKIPIKI N.K. HATA HIVYO WATUHUMIWA MBALIMBALI WALIKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI AMBAPO BAADHI YA  KESI ZIMEMALIZIKA NA NYINGINE ZIPO KATIKA HATUA MBALIMBALI.

KATIKA KIPINDI CHA JAN-JUNI, 2014 JUMLA YA MAKOSA YOTE YA JINAI YALIYORIPOTIWA KUTOKEA YALIKUWA 13,481, IKILINGANISHWA NA MATUKIO 13,670 YALIYORIPOTIWA KUTOKEA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013, HIVYO KUNA PUNGUFU YA MATUKIO 189, SAWA NA ASILIMIA 2 [2%].


KWA UPANDE WA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI JUMLA YA  MATUKIO YOTE YALIYORIPOTIWA KATIKA KIPINDI CHA JAN-JUNI, 2014  IKIWEMO MATUKIO YA AJALI NA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA USAFIRISHAJI YALIKUWA 26,668 WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 YALIKUWA 25,266 HIVYO KUNA ONGEZEKO LA MATUKIO 1,402 SAWA NA ASILIMIA 4 [4%] MATUKIO YA  AJALI YALIYORIPOTIWA KIPINDI CHA JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 197 WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 YALIKUWA 266 HIVYO KUNA PUNGUFU YA  MATUKIO 69 SAWA NA ASILIMIA 26 [26%].

AJALI ZA VIFO ZILIZORIPOTIWA KIPINDI CHA JAN-JUNI 2014 ZILIKUWA 112 WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 ZILIKUWA 128 HIVYO KUNA PUNGUFU YA MATUKIO 16 SAWA NA ASILIMIA 13 [13%]. WATU WALIOKUFA KIPINDI CHA JAN-JUNI 2014 WALIKUWA 130 WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 WALIKUWA 157 HIVYO KUNA PUNGUFU YA WATU 27 SAWA NA ASILIMIA 18 [18%].

AJALI ZA MAJERUHI ZILIZORIPOTIWA KIPINDI CHA JAN-JUNI 2014 ZILIKUWA 85 WAKATI MWAKA 2013 ZILIKUWA 138 HIVYO KUNA PUNGUFU YA AJALI 53 SAWA NA ASILIMIA 39 [39%]. WATU WALIOJERUHIWA JAN-JUNI 2014 WALIKUWA 245 WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 WALIKUWA 455 HIVYO KUNA PUNGUFU YA WATU 210 SAWA NA ASILIMIA 47 [47%].

MAKOSA YA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA USAFIRISHAJI KATIKA KIPINDI CHA JAN-JUNI 2014 YALIKUWA   26,471 WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 YALIKUWA 24,967 HIVYO KUNA ONGEZEKO LA MAKOSA 1,504 SAWA NA ASILIMIA 6 [6%]. TOZO LILILOKUSANYWA KUTOKA KWA MAKOSA [NOTIFICATION] KWA KIPINDI CHA JAN-JUNI 2014 LILIKUWA TSHS 705,780,000/= IKILINGANISHWA NA TSHS 654,740,000/= KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 HIVYO KUNA ONGEZEKO LA TSHS 51,040,000/=, SAWA NA ASILIMIA 8 [8%], HIVYO KUUFANYA MKOA WA MBEYA KUWA MIONGONI MWA MIKOA ILIYOONGOZA KWA UKUSANYAJI  TOZO NCHINI.


MAKOSA KERO KWA JAMII.

JUMLA YA MATUKIO AMBAYO NI KERO KWA JAMII YALIYORIPOTIWA MKOA WA MBEYA KWA KIPINDI CHA JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 2,567 WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 YALIKUWA 2,683 HIVYO KUNA PUNGUFU YA  MATUKIO 116 SAWA NA ASILIMIA 5 [5%].

KATIKA KIPINDI CHA JAN-JUNI 2014, MATUKIO YA MAUAJI YALIKUWA 135 WAKATI MWAKA 2013 YALIKUWA 156 KUNA PUNGUFU YA MATUKIO 21 SAWA NA ASILIMIA 14 [14%], KUBAKA JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 252 MWAKA 2013 YALIKUWA 197 HIVYO KUNA ONGEZEKO LA MATUKIO 55 SAWA NA ASILIMIA 28 [28%].

MATUKIO YA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 4 MWAKA 2013 YALIKUWA 5 KUNA PUNGUFU YA  TUKIO 1,SAWA NA ASILIMIA 20.UNYANG’ANYI WA KUTUMIA NGUVU JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 61 MWAKA 2013 YALIKUWA 89 KUNA PUNGUFU YA  MATUKIO 28,SAWA NA ASILIMIA 32 [32%].

MATUKIO YA UVUNJAJI JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 180, MWAKA 2013 YALIKUWA 202, KUNA PUNGUFU YA MATUKIO 22, SAWA NA ASILIMIA 11. WIZI WA MIFUGO JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 126, MWAKA 2013 YALIKUWA 102, KUNA ONGEZEKO LA MATUKIO 24, SAWA NA ASILIMIA 24 [24%]. WIZI WA PIKIPIKI JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 96 MWAKA 2013 YALIKUWA 69, KUNA ONGEZEKO LA MATUKIO 27, SAWA NA ASILIMIA 40. MATUKIO YA WIZI JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 1,713 MWAKA 2013 YALIKUWA 1,863 YALIKUWA 150, SAWA NA ASILIMIA 8 [8%].


MATUKIO YATOKANAYO NA JITIHADA ZA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU NA WANANCHI WENGINE.

JUMLA YA  MAKOSA 282 YALIRIPOTIWA KIPINDI CHA JAN-JUNI,2014, IKILINGANISHWA NA MATUKIO 244, MWAKA 2013, HIVYO KUNA ONGEZEKO LA MATUKIO 38, SAWA NA ASILIMIA 16 [16%].

MATUKIO YA  KUPATIKANA NA BHANGI JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 130, MWAKA 2013 YALIKUWA 124, HIVYO KUNA ONGEZEKO LA MATUKIO 6, SAWA NA ASILIMIA 5. POMBE YA  MOSHI [GONGO] JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 86, KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 YALIKUWA 50, KUNA ONGEZEKO LA MATUKIO 36, SAWA NA ASILIMIA 72. KUPATIKANA NA SILAHA JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 19, KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 YALIKUWA 15, KUNA ONGEZEKO LA MATUKIO 4, SAWA NA ASILIMIA 27 [27%].

MATUKIO YA KUKAMATWA WAHAMIAJI HARAMU JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 14, KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 YALIKUWA 36, KUNA PUNGUFU  YA  MATUKIO 22, SAWA NA ASILIMIA 62 [62%]. KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI  JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 8, KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013 YALIKUWA 12, KUNA PUNGUFU YA MATUKIO 4, SAWA NA ASILIMIA 34 [34%]. KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA JAN-JUNI 2014 YALIKUWA 1, SAWA NA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013. AIDHA MAFANIKIO HAYA YALITOKANA NA USHIRIKIANO MZURI ULIOPO KATI YA JESHI LA POLISI, WADAU NA  WANANCHI MBALIMBALI.

MAFANIKIO.

BAADHI YA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA NI PAMOJA NA:-
·         KUPUNGUA KWA UHALIFU KWA ASILIMIA 2.
·         KUPUNGUA KWA MATUKIO YA  MAUAJI YATOKANAYO NA IMANI  POTOFU ZA KISHIRIKINA, KUTOKA MATUKIO 32, JAN- JUNI- 2013 NA KUFIKIA MATUKIO 23, JAN-JUNI, 2014, SAWA NA ASILIMIA  29.

JUMLA YA WAHAMIAJI HARAMU 195 WALIKAMATWA WAKIWEMO:-
(i)                 Waethiopia   - 152
(ii)               Wasomalia    - 10
(iii)             Pakistan -  7
(iv)             Burundi – 23
(v)               Malawi – 2
(vi)             Msumbiji 1.

·         POMBE HARAMU YA MOSHI {GONGO} YENYE UJAZO WA LITA 479 PAMOJA NA MITAMBO 16 ILIKAMATWA.
·         BHANGI YENYE UZITO WA KGM 296 NA GRAM 678, MICHE 314 PAMOJA NA MASHAMBA MATATU YA BHANGI YENYE UKUBWA WA JUMLA YA EKARI MOJA NA ROBO YALIKAMATWA.
·         MIRUNGI UZITO WA GRAM 500 ILIKAMATWA.
·         SILAHA /BUNDUKI 19 ZILIKAMATWA KATI YA HIZO GOBOLE 15, BASTOLA 2 ZA KIENYEJI, RIFFLE 1 NA S/GUN 1. PIA SILAHA MBILI ZILIKAMATWA BAADA YA MAJAMBAZI KUUAWA KATIKA JARIBIO LA KUFANYA UNYANY’ANYI. SILAHA HIZO NI SMG N0-3514 NA AK-47 N0- 592058 NA RISASI 25 KWENYE MAGAZINE.
·         MAFUTA AINA YA DIESEL UJAZO WA LITA 3,265 MALI YA WIZI ILIKAMATWA.
·         NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA TSHS 1,700,000/= NA USD 2,130 ZILIKAMATWA.



CHANGAMOTO.

PAMOJA NA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA, LAKINI BADO KUNA CHANGAMOTO ZINAZOLIKABILI JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA. MIONGONI MWA CHANGAMOTO HIZO NI:

  • BADO BAADHI YA WANACHAMA WA VYAMA /VIONGOZI WA SIASA HAWAJAONA UMUHIMU WA KUTII SHERIA WAO WENYEWE NA KUENDELEA KUTOA MANENO YA KUWAGAWA WANANCHI.
§  BAADHI YA WANANCHI WANAENDELEA KUFICHA WAHALIFU NA UHALIFU KATIKA MAENEO YAO NA KUSHINDWA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI.
§  BADO MAKOSA YA KUBAKA, WIZI WA MIFUGO NA WIZI WA PIKIPIKI YAMEONGEZEKA KIPINDI CHA JAN-JUNI, 2014 IKILINGANISHWA NA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2013. HATA HIVYO MIKAKATI INAFANYWA ILI KUPUNGUZA/KUDHIBITI MATUKIO HAYO.

§  LICHA YA  MAKOSA YA  MAUAJI  KUPUNGUA KUTOKA 156 JAN - JUNI, 2013  NA KUFIKIA 135  JAN - JUNI, 2014, LAKINI MATUKIO  23  YALITOKANA NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA [UCHAWI], MATUKIO 33 YALITOKANA NA  WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI, MATUKIO 16 YALITOKANA NA UGOMVI MAJUMBANI, MATUKIO 11 UGOMVI VILABUNI, MATUKIO 20 WIVU/UGONI, MATUKIO 9 KISASI NA MATUKIO 23 SABABU NYINGINEZO.
WITO WA KAMANDA:

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI NINATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI HASA KWA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU/WAHALIFU MAPEMA ILI KUZUIA MATUKIO YA UHALIFU NA KIUHALIFU YASITOKEE.

AIDHA NINATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUZINGATIA UTOAJI WA MALEZI BORA KWA WATOTO/VIJANA ILI WAKUE KATIKA MISINGI MIZURI YA MAADILI MEMA KIJAMII NA KUJIEPUSHA NA MATUKIO YA KIUHALIFU/KUKATAA UHALIFU WANGALI WADOGO IKIWA NI PAMOJA NA KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA, KUCHEZA KAMARI N.K.
           
HALIKADHARIKA, KATIKA KUHAKIKISHA UHALIFU UNAPUNGUA, VYOMBO VYA HABARI VINA NAFASI YAKE KATIKA JAMII IKIWA NI PAMOJA NA KUENDELEA KUTOA ELIMU MBALIMBALI ZA KIULINZI NA USALAMA KWA KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA MBALIMBALI. AIDHA KWA KUTAMBUA MAZINGIRA TULIYONAYO NA CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA MKOA WETU, KILA MMOJA WETU AONE KILA SABABU YA KUFIKISHA UJUMBE/TAARIFA YENYE KUKEMEA/KUPINGA NA KULETA MABADILIKO CHANYA KATIKA JAMII KWA LENGO LA KULETA AMANI NA UTULIVU.

KWA KUTAMBUA KUWA SUALA LA ULINZI NA USALAMA UNAANZIA NGAZI YA FAMILIA, KIJIJI, KITONGOJI, KATA, TARAFA, WILAYA HADI NGAZI YA MKOA, NI VYEMA KILA MMOJA WETU KUTAMBUA NA KUAMINI USALAMA WA MALI NA MAISHA YETU UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE. KWA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA WETU NA MALI ZETU INATOA FURSA KWA WAWEKEZAJI KUWEKEZA KATIKA MKOA WETU, WANANCHI KUJIAJIRI NA KUAJIRIWA IKIWA NI PAMOJA NA KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII BILA KUATHIRI AMANI NA UTULIVU.



Imetolewa na:
 [AHMED Z. MSANGI – SACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »