TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


“PRESS RELEASE” TAREHE 01. 08. 2013.


WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI

MNAMO TAREHE 31.07.2013 MAJIRA YA SAA 03:30HRS HUKO KIJIJI CHA ILINGA KATA YA KATUMBA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA, REBEKA D/O KIKONYOLE, MIAKA 90, MNYAKYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI HAPO ALIVAMIWA NDANI YA NYUMBA YAKE KISHA KUCHUKULIWA/KUTEKWA MPAKA KICHAKANI AMBAKO ALIKATWA NA KITU KINACHODHANIWA KUWA NI SHOKA KATIKA PAJI LAKE LA USO NA KUFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANA, CHANZO CHA MAUAJI HAYO KINACHUNGUZWA. MSAKO MKALI WA KUWASAKA WALOHUSIKA NA TUKIO HILI UNAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA. PIA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE KWENYE MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

WILAYA YA MBARALI – AJALI YA PIKIPIKI KUANGUKA NA KUSABABISHA  
                                          KIFO

MNAMO TAREHE 31.07.2013 MAJIRA YA SAA H16:00HRS UKO KIJIJI CHA IYULA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA, PIKIPIKI NO T. 695 AVP AINA YA KIN FAN IKIENDESHWA NA BEBO S/O KEYA, MIAKA 22, MMASAI, MKULIMA NA MKAZI WA MWANAVALA ILIACHA NJIA KISHA KUANGUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA ABIRIA WAKE AITWAYE LAYO S/O KEYA, MIAKA 24, MMASAI MKULIMA NA MKAZI WA MWANAVALA, CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEMKAMATWA NA   TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAANDALIWA.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO HUSUSANI MADEREVA PIKIPIKI [BODABODA] KUWA NA TAHADHARI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA. 

WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA GONGO [POMBE MOSHI]

MNAMO TAREHE 31/07/2013 MAJIRA YA  SAA 04:00HRS HUKO SOKOMATOLA JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA KAIZERI S/O SANGA, MIAKA 28, MKINGA,  MKAZI WA MAMA JOHN AKIWA NA POMBE MOSHI 1/3 LITA KWENYE CHUPA YA  KONYAGI. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA GONGO HIYO AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAANDALIWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO]  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.



WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI

MNAMO TAREHE 31/07/2013 MAJIRA SAA 02:30HRS SIDO MWANJELWA JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA KEFA S/O PATSON, MIAKA 25, MSAFWA MKULIMA NA MKAZI WA MWANJELWA  AKIWA NA BHANGI  KETE TANO SAWA NA GRAMU 25 NDANI YA  MFUKO WA SURUALI. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI HIYO AMAEKAMATWA NA UTARATIBU WA KUMFIKISHA MAHAKKAMANI UNAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


Imesainiwa na,
[DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »