TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 14.07.2014.
·
MTEMBEA KWA MIGUU MMOJA MKAZI WA MAFIATI JIJINI
MBEYA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
·
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA SHULE YA
SEKONDARI IWAMBALA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PETER
MADZANILE (31) RAIA NA MKAZI WA
NCHINI ZIMBABWE AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI IT 6216 AINA YA TOYOTA SPACIO ALIYOKUWA AKIENDESHA KUGONGANA NA GARI YENYE NAMBA ZA
USAJILI STK 5988 AINA YA TOYOTA LAND CRUISER S/WAGON AMBULANCE
MALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA RASHID KAPOMBE (37) MKAZI WA MBARALI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE MNAMO TAREHE 13.07.2014 MAJIRA YA SAA
05:00 ALFAJIRI KATIKA KIJIJI CHA MAENGELE, KATA NA TARAFA YA ILONGO, WILAYA
YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
AIDHA KATIKA
AJALI HIYO, DEREVA WA GARI STK 5988,
RASHID KAPOMBE PAMOJA NA ABIRIA WAKE
DORAH MWASHILANGA (32) MKAZI WA MBARALI WALIJERUHIWA NA
WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI
WA MAGARI YOTE MAWILI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MISHENI
CHIMALA NA MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MAX SIMBEYE
(60) MKAZI WA MAFIATI AMEFARIKI
DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU
BAADA YA KUGONGWA NA GARI AMBALO HALIKUWEZA KUFAHAMIKA WALA DEREVA WAKE.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO 13.07.2014 MAJIRA YA
SAA 12:30 MCHANA KATIKA ENEO LA MAFIATI, KATA YA MANGA, TARAFA YA SISIMBA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA, BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI BADO
KINACHUNGUZWA, DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI NA JUHUDI ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE,
VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWANAFUNZI WA
KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI IWAMBALA - UYOLE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FROLA ASUKILE (14) MKAZI WA UYOLE
AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA
USAJILI T.361 AQK AINA YA SUZUKI
ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.
TUKIO HILO
LIMETOKEA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU MNAMO TAREHE 13.07.2014 MAJIRA YA SAA
17:45 JIONI KATIKA ENEO LA UYOLE YA KATI, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA
IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO
CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI,
JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE,
VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
Imetolewa:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon