TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 15.07.2014.
·
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MKUTANO
AMEMUUWA MUME WAKE KWA KUMPIGA KWA KIPANDE CHA MTI.
·
WATU
WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA MBALIMBALI.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MKUTANO
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MIRIANA
SIMTOWE (32) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA ZA
KUMUUWA MUME WAKE AITWAYE PETRO MTEKA
(33) MKAZI WA KIJIJI CHA MKUTANO KWA KUMPIGA KWA KIPANDE CHA MTI.
INADAIWA KUWA MNAMO TAREHE 13.07.2014 MAJIRA YA SAA
21:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MKUTANO. KATA YA NZOKA, TARAFA YA NDALAMBO,
WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA MTUHUMIWA AKIWA NJIANI NA MAREHEMU MUME WAKE
WAKITOKEA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI WAKIWA WAMELEWA ILITOKEA HALI YA
KUTOELEWANA [UGOMVI] NA NDIPO MTUHUMIWA ALIPO TUMIA KIPANDE CHA MTI NA KUMPIGA
NACHO MUME WAKE NA KUMSABABISHIA MAJERAHA.
KUTOKANA NA MAJERAHA ALIYOKUWA AMEYAPATA MWANAUME
HUYO, ALIPELEKWA KATIKA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MKUTANO KWA MATIBABU NA
ALIFARIKI DUNIA MNAMO TAREHE 14.07.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA UNYWAJI WA POMBE KUPITA KIASI KWANI NI
HATARI KWA AFYA ZAO NA HULETA MADHARA KATIKA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA WANA
NDOA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUPATA
MUAFAKA.
TAARIFA
ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WATATU 1. JOSEPH
MWAKAPASA (20) 2. GWAKISA MWANDOBO
(30) NA 3. MUSSA ABELI (31) WOTE
WAKAZI WA USHIRIKA –TUKUYU WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA
1 ½ .
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.07.2014
MAJIRA YA SAA 10:40 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MPUGUSO, TARAFA YA
PAKATI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO.
KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA JOHN DAUD (43) MKAZI WA USHIRIKA
–TUKUYU ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE 14
SAWA NA UZITO WA GRAM 70.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.07.2014 MAJIRA YA
SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MPUGUSO, TARAFA YA PAKATI,
WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI PAMOJA NA BHANGI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na;
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon