Ukeketaji kwa Wanawake na Madhara yake

Ukeketaji kwa wanawake husababisha maumivu makali na madhara ya  kisaikolojia ambayo hudumu kwa muda mrefu.


Ukeketaji wa wanawake ni kitendo kinachohusisha  kuondolewa kwa kinembe, midomo ya ndani-na-nje ya uke, na au  kushona  kwa pamoja pande z mbili zamashavu ya uke na kuacha tu shimo dogo kwa ajili ya kupita mkojo na damu ya hedhi. Kwa kawaida ukeketaji unafanywa kwa kutumia wembekwa wasichana wenye umri kati ya miaka  nne na 12, bila dawa ya ganzi.

Kuna aina tatu za ukeketaji. Aina ya kwanza ya  ukeketaji moja ni sawa na kuondoa korodani kwa  mwanaume, wakati  aina ya tatu ni sawa na kuondoa  makende na uume kwa pamoja.

Ukeketaji unaweza kusababisha kutokwa damu nyingi, maumivu, kukosa hisia, matatizo wakati wa kujifungua, utasa, maumivu makali wakati wa ngono, maambukizi ya mara kwa mara na kuziba kwa mkojo. Na katika baadhi ya matukio inasababisha kifo. Tofauti na tohara kwa wanaume, ukeketaji kwa wanawake pia inaondoa raha wakati wa kufanya mapenzi.

Hakuna shaka yoyote kuwa ukuNi  ukeketaji hauna faida yoyote  kiafya na  wakati mwingine upasuaji unahitajika ili kurekebisha uke.
Previous
Next Post »