Tazama Video Justin Bieber aomba radhi kwa utani wa ubaguzi wa rangi alioufanya akiwa mtoto


Justin Bieber alijikuta katika tanuru la moto wa jamii hii inayopiga kwa nguvu zote ubaguzi wa rangi baada ya video inayomuonesha akitoa maneno ya kibaguzi alipokuwa na umri wa miaka 15 kuvuja kupitia mtandao wa TMZ.
Katika video hiyo, Justin anaonekana akiuliza kwa mzaha, “Why are black people afraid of chain saws?  Na baadae anajibu swali hilo mwenyewe, “Run n**ga,n**ga, n**ga, ga, n**ga.”  
TMZ imeeleza kuwa iliipata video hiyo miaka mingi iliyopita lakini iliitunza kwa kuzingatia umri wa Justin Bieber kwa kipindi hicho.
Mwimbaji huyo ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 20, ameomba radhi huku akieleza kuwa  alikuwa mtoto na hakujua nguvu ya maneno hayo na jinsi ambavyo yangeumiza.
“Kama kijana mdogo, sikuelewa nguvu ya maneno fulani na jinsi ambavyo yanaweza kuumiza. Nilifikiria ilikuwa sawa turudia maneno hatari na utani, lakini sikutambua kwa wakati huo kuwa haukuwa kitu cha ucheshi na hakika matendo yangu yaliendeleza ujinga wangu.” Bieber amesema katika tamko lake.
“Inachukua urafiki wangu kwa watu wa tamaduni zote kwa umakini na ninaomba radhi kwa kuwakosea au kumuumiza mtu yoyote kwa maneno yangu ya kitoto. Nilikuwa mtoto wakati ule na hivi sasa ni mwanaume ambaye nafahamu wajibu wangu kwa dunia kutofanya kosa hilo tena.” Ameongeza.
Justine ameendeea;
“Ujinga hauna nafasi katika jamii yetu na natumaini kushare makosa yangu kutawafanya wengine kutofanya makosa kama haya kwa siku za usoni. Nilifikiria kwa urefu kuhusu kile nilichotaka kusema lakini kusema ukweli ndicho kitu sahihi daima.”
Justine amemaliza kwa kusema miaka mitano iliyopita alifanya kosa la kitoto na kuwashukuru watu waliokuwa karibu nae kwa kumsaidia kujifunza kama kijana.
“Once again…. I’m sorry.” Amefunga tamko lake.
Video hiyo ilipotoka ilimuongezea Justin Bieber orodha ya makosa ambayo ameonekana akiyafanya ukubwani huku akikabiriwa na mashitaka mbalimbali katika mahakama za Marekani na Canada.
Previous
Next Post »