KUMBE TABIA HII YA USANYANYAJI KWA WAGONJWA SI TANZANIA TU SOMA HAPA NI MWAMKE ALIYEFARIKI DUNIA NDANI YA HOSPITALI WAKATI AKIPIGA MAGOTI ILI APATIWE DAWA


mwanamke
Unaweza kudhani matukio haya hutokea katika hospitali za kawaida tu. Hii ni ya kusikitisha zaidi na imetokea katika hospitali kubwa nchini Uingereza. Picha hii ya mwisho inamuonyesha mwanamke mmoja aliyekuwa amezidiwa hospitali na akashindwa kupatiwa dawa hadi kuamua kupiga magoti hospitali akibembeleza apatiwe dawa ya maumivu tu kutokana na kuzidiwa kwake lakini wauguzi hawakumsaidia chochote hadi umauti ulimkuta.

mwanamke2
Siku mbili baada ya kutelekezwa na maafisa wa hospitali, mwanamama huyo Margaret Lamberty alipoteza maisha baada ugonjwa wake unaotibika kumzidi kutokana na kushindwa kupatiwa msaada.

Margaret alifikishwa hospitali ya chuo kikuu cha A&E North Staffordshire nchini Uingereza na wanafamilia yake akiwa na maumivu makali ya tumbo, Mtoto wake kike aitwaye Laura amesema kuwa baada ya kufika hospitalini hapo wauguzi walikuwa wakimuangalia tu bila kumpa msaada wowote ndipo mama yake akaamua hadi kupiga magoti akiwaomba wampatie dawa ya maumivu lakini hakusikilizwa na mtu.
mwanamke3
Hospitali hiyo imekumbwa na kashfa kubwa kwa sasa baada ya kifo cha mwanamke huyo ambapo familia inapanga kuishtaki kwa kushindwa kutimiza wajibu wao hadi kusababisha kifo cha ndugu yao.
Previous
Next Post »