MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI
JANGURUTU DARASA LA TANO ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HABIBU DISMASS (11)
AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI
T.120 AMV AINA YA CAMRY LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DERAVA OTINO MWAMPAMBA (48)
MWALIMU SHULE YA SEKONDARI, MBARALI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
08.05.2014 MAJIRA YA SAA 16:15 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MABANDA, KATA NA TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA
AJALI NI MWENDO KASI. DEREVAAMEKAMATWA NA GARI LIPO POLISI-RUJEWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUTEMBEA PEMBENI
MWA BARABARA NA KUVUKA SEHEMU ZENYE VIVUKO ILI KUEPUKA AJALI.
Imetolewa
na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon