BIBI WA MIAKA 69 AUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI.


BIBI WA MIAKA 69 MKAZI WA KATABE WILAYA YA RUNGWE AITWAYE AIDA MWANGOSIM AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI NA USONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA NYUMBANI KWAKE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:30 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KATABE, KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE   WILAYA YA RUNGWE   MKOA WA MBEYA. AIDHA KATIKA TUKIO HILO HAWA GEORGE (12) MWANAFUNZI  SHULE YA MSINGI KATABE DARASA LA PILI AMBAYE NI MJUKUU WA MAREHEMU ALIJERUHIWA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI KISHA KUBAKWA NA AMELAZWA HOSPITALI YA  MAKANDANA-TUKUYU.
CHANZO CHA TUKIO KINACHUNGUZWA, NDANI YA NYUMBA YA  MAREHEMU KUMEKUTWA SHOKA NA JIWE MOJA KUBWA AMBAVYO  VINADHANIWA KUTUMIKA KATIKA TUKIO HILO. UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOWAACHA WAJANE/WAZEE WENYE UMRI MKUBWA NA WATOTO WADOGO BILA UANGALIZI WA KARIBU ILI KUEPUSHA WATU WENYE NIA MBAYA/WAHALIFU KUTOPATA NAFASI YA KUTEKELEZA UHALIFU WAO. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE/WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


Previous
Next Post »