MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI NA WENGINE WATATU KUJERUHIWA




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 17.05.2014.

Ø  MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KUFUATIA  AJALI YA  MOTO


Ø  MTU  MMOJA  AFARIKI  DUNIA KATIKA AJALI NA WENGINE WATATU KUJERUHIWA

Ø  JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAMSHIKILIA MTU MMOJA   KWA KUKUTWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO].

TUKIO LA KWANZA.

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KUFUATIA   AJALI YA  MOTO.

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA THOBIAS LUGOYA [68], MKAZI WA KIJIJI CHA UTURO, ALIFARIKI DUNIA BAADA YA  NYUMBA YAKE KUUNGUA MOTO HUKU AKIWA AMELALA PEKE YAKE NDANI YA  NYUMBA YAKE.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 16.05.2014 MAJIRA YA  SAA 00:30HRS USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA UTURO, KATA YA  IGURUSI, TARAFA YA  ILONGO,WILAYA YA  MBARALI, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA  MAJANGA YA  MOTO ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

TUKIO LA PILI.


MTU  MMOJA  AFARIKI  DUNIA KATIKA AJALI NA WENGINE WATATU KUJERUHIWA.


MTU MMOJA  GASPER SAANANE [40], MKAZI WA KANTAWA- NAMANYELE- SUMBAWANGA ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO KUFUATIA AJALI  YA  MAGARI MAWILI KUGONGANA NA KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 16.05.2014 MAJIRA YA  SAA 08:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA OLD-VWAWA,  KATA NA TARAFA YA  VWAWA, WILAYA YA  MBOZI,  MKOA WA MBEYA, BARABARA KUU YA  MBEYA/ TUNDUMA. KATIKA TUKIO HILO  GARI IT 3456 AINA YA  TOYOTA IPSUM LIKIENDESHWA NA DEREVA ABDALLAH  ALLY [40] MKAZI WA TANDIKA – DSM  KULIGONGA GARI T. 259 BZU/T.819 BAB AINA YA  FAW LORI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA  ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MATHIUS JACKSON. AIDHA KATIKA TUKIO HILO  WATU WENGINE WATATU WALIJERUHIWA AKIWEMO DEREVA ABDALLAH ALLY,  WENGINE NI  DISMAS LINDA [40],  MKAZI WA SUMBAWANGA NA  HUSNA MASOUD [28],  MKAZI WA BUGURUNI DSM . CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA DEREVA WA GARI IT 3456.

MAJERUHI WOTE WATATU WAMELAZWA HOSPITALI YA  SERIKALI VWAWA-MBOZI NA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI DEREVA AFIKISHWE MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOYUMIA VYOMBO VYA USAFIRI KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. 

KATIKA MSAKO.

JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAMSHIKILIA MTU MMOJA  KUTOKANA NA MISAKO MBALIMBALI ILIYOFANYIKA.  KATIKA TUKIO  HILO   JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA  PILLY KAPOJA [45], MKAZI WA KAFUNDO- IPINDA  KWA KOSA LA KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 12.   TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 16.05.2014 MAJIRA YA  SAA 13:35HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAFUNDO-IPINDA, KATA YA   IPINDA,  TARAFA YA  NTEBELA, WILAYA YA  KYELA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA  NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.





Signed by

 [ AHMED Z. MSANGI – SACP ].

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »