WATOTO WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MOTO ILIYOTOKEA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.


WATOTO WAWILI WALIOTAMBULIWA KWA MAJINA YA 1. BARAKA LACKSON (04) NA 2. ESTER LACKSON (02) NA MIEZI 10 WAMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MOTO ILIYOTOKEA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI BAADA YA NYUMBA WALIMOKUWA WAKIISHI KUUNGUA MOTO.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.05.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO KATIKA MTAA WA MAGEUZI MJI MKONGWE, KATA YA  NSALAGA, TARAFA YA  UTENGULE USONGWE, WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI , MKOA WA MBEYA. AIDHA MTOTO MARTIN KABWILILE (09) ALIJERUHIWA KWA KUUNGUA MOTO MIGUUNI   NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO NI MSHUMAA ULIOKUWA UMEWASHWA NA WAHANGA CHUMBANI  NA WAO KULALA.
MOTO ULIZIMWA NA WANANCHI KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI POLISI. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA IFISI. WAKATI WA TUKIO WAZAZI HAWAKUWEPO NYUMBANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WADOGO NA KUCHUKUA TAHADHARI KUTOKANA NA MAJANGA YATOKANAYO NA MOTO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA. AIDHA NI VYEMA KUACHA MTU WA KUWAANGALIA WATOTO PINDI WANAPOKWENDA KATIKA SHUGHULI ZAO NA KUHAKIKISHA VITU KAMA MISHUMAA, VIBATARI NA MAFUTA YA DIESEL NA PETROL VINAWEKWA MBALI NA WATOTO KWANI NI HATARI.
Previous
Next Post »