Watu 682 wahukumiwa kifo nchini Misri, wengine 492 wavuliwa kitanzi, ndugu zao wazirai

Jaji wa mahakama ya Misri amewahukumu kifo watu 683 walitajwa kuwa wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood baada ya kukutwa na hatia katika makosa ya kushambulia kituo cha polisi mjini Minya mwaka jana ambapo polisi mmoja alikufa.
Kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood, Mohammed Badie ni miongoni mwa watu hao waliohukumiwa kifo ambapo ilielezwa kuwa vurugu walizoanzisha zilisababisha watu wengi kupoteza maisha.
Ripoti zinasema kuwa jamaa wa watuhumiwa waliokuwa wanasubiri nje ya mahakama walizirai baada ya kupokea taarifa za hukumu hiyo.
Katika hatua nyingine, Jaji wa mahakama hiyo pia amebatilisha hukumu ya kifo iliyotolewa kwa watu 492 kati ya watu 529. Hukumu hiyo ilipitishwa mwezi uliopita na watu hao wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu limekosoa vikali mwenendo wa kesi hiyo na hukumu iliyotolewa ambapo imedaiwa kuwa kesi hizo zilisikilizwa masaa machache huku mahakama ikiwazuia mawakili kuwawakilisha washitakiwa.
Previous
Next Post »