TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 12.04.2014.
- WATU 37 WAKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA FUJO NA KUHARIBU MALI.
- MTU MMOJA AKUTWA AMEJIUA CHUMBANI KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA WA NCHINI ETHIOPIA BAADA YA KUKAMATWA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU 37 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA FUJO NA KUHARIBU MALI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA TAREHE 11.04.2014 MAJIRA
YA SAA 10:30 ASUBUHI HUKO KATIKA ENEO LA IYELA - AIRPORT, KATA YA
IYELA, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA
MKOA WA MBEYA AMBAPO KUNDI LA WATU WAKIWEMO WAENDESHA PIKIPIKI MAARUFU
KWA JINA LA BODABODA ZAIDI YA MIA MBILI
WALIVAMIA KWENYE MSIBA WA MAREHEMU SIZA
JOHN MWAMBENJA [28] MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA, MKAZI WA
AIRPORT NA KUFANYA FUJO IKIWA NI PAMOJA
NA KUHARIBU MALI MBALIMBALI KATIKA NYUMBA HIYO WAKISHINIKIZA KUMKAMATA MTALAKA
WA MAREHEMU OLIVA HERODE MWAMLIMA [
25] MKAZI WA FOREST MPYA AMBAYE ALIKUWEPO KATIKA MSIBA HUO KWA MADAI KUWA
ANAHUSIKA NA NJAMA ZA MAUAJI YA
ALIYEKUWA MUME WAKE KUTOKANA NA KUACHWA KWA SABABU ZA MATATIZO YA KIFAMILIA.
MAREHEMU SIZA JOHN MWAMBENJA ALIUAWA NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA NA MWILI WAKE KUKUTWA UMETUPWA KANDO YA RELI YA TAZARA TAREHE 09.04.2014 UKIWA NA JERAHA LA KUCHOMWA
NA KITU CHENYE NCHA KALI SHINGONI NA KANDO YAKE KUTELEKEZWA PIKIPIKI YAKE MPYA YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 932 CTZ AINA YA KINGLION. KUFUATIA VURUGU HIZO ZILIZOZIMWA NA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA, WATU 37 WALIKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMA YA MWANZO
MBEYA MJINI AMBAO WALISOMEWA MASHITAKA YAO SHAURI LA JINAI NAMBA 291/2014.
WATUHUMIWA WOTE WAMEPELEKWA MAHABUSU GEREZA LA RUANDA AMBAPO KESI
ITAANZA KUSIKILIZWA 14.04.2014.
AIDHA KATIKA
VURUGU HIZO MALI ZA JESHI LA POLISI GARI MOJA LA KITUO CHA POLISI KATI 474 AINA YA
LAND ROVER 110 LILIHARIBIWA KWA KUPIGWA
MAWE NA KUVUNJWA KIOO KIKUBWA CHA MBELE. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU
YALIYORIPOTIWA KUTOKEA WAKATI WA VURUGU HIZO NA HALI YA AMANI ILIREJEA KUWA YA KAWAIDA
NA WANANCHI WANAENDELEA NA SHUGHULI ZAO KAMA KAWAIDA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE
WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANOWAKAMATA KWA
TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE. AIDHA ANATOA RAI
KWA JAMII KUJENGA TABIA YA KUHESHIMU
MAMLAKA ZILIZOWEKWA KISHERIA IKIWA NI PAMOJA NA VYOMBO VYA DOLA ILI KUEPUKA
MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA BADALA YA KULETA USHINDANI NA VURUGU. PIA KAMANDA
MSANGI AMESISITIZA KUWA JESHI LA POLISI HALITASITA KUWAKAMATA NA KUWACHUKULIA
HATUA KALI ZA KISHERIA WALE WOTE WANAOKAIDI NA KULETA VURUGU.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MFANYABIASHARA
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JAIL
RUBANGE [57] MKAZI WA WILAYA YA KYELA ALIKUTWA AMEJIUA KWA KUJICHOMA KISU
SHINGONI KATIKA CHUMBA ALICHOPANGA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA HUKO KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO TEN COMMANDMENT ILIYOPO
ENEO LA STENDI KUU KATA NA TARAFA YA
SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA TAREHE 11.04.2014 MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI.
CHANZO CHA
TUKIO HILI BADO KINACHUNGUZWA, INGAWA
UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA MAREHEMU
ALIKUWA ANASUMBULIWA NA MARADHI YA
KISUKARI NA BP KWA MUDA MREFU. MAREHEMU ALICHUKUA CHUMBA TAREHE 10.04.2014 MAJIRA YA SAA 16:00
JIONI NA ALIFANYA KITENDO HICHO
BAADA YA KUJIFUNGIA KWA NDANI KATIKA CHUMBA NAMBA 13 KISHA
KUJIUA NA KISU. KISU ALICHOKITUMIA KIJIUA KILIKUTWA BADO KIPO SHINGONI. AIDHA MAREHEMU HAKUACHA UJUMBE WOWOTE. MWILI
WAKE ULIKUTWA NDANI KATIKA BAADA YA ASKARI POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WENYE
NYUMBA KUVUNJA MLANGO.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI INA MADHARA
KWA JAMII.
NA
KATIKA TUKIO LA TATU:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU
WAWILI 1. LILE
RAMA [20] NA 2. MESFIN HABTE [22]
WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
WATU HAO WALIKAMATWA TAREHE 11.04.2014 MAJIRA YA SAA 22:00
USIKU KATIKA ENEO LA POSTA TUNDUMA,
KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA
JESHI LA POLISI.
TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA
SHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA NI PAMOJA
NAA RAIA WA KIGENI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon