MTU MMOJA AKUTWA AMEJIUA CHUMBANI KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI.





MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JAIL RUBANGE [57] MKAZI WA WILAYA YA KYELA ALIKUTWA AMEJIUA KWA KUJICHOMA KISU SHINGONI KATIKA CHUMBA ALICHOPANGA.

TUKIO HILO LIMETOKEA   HUKO KATIKA NYUMBA YA  KULALA WAGENI IITWAYO TEN COMMANDMENT ILIYOPO ENEO LA STENDI KUU KATA NA TARAFA YA  SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA TAREHE 11.04.2014 MAJIRA YA  SAA 10:30 ASUBUHI.

CHANZO CHA TUKIO HILI BADO  KINACHUNGUZWA, INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI  UNAONYESHA MAREHEMU ALIKUWA ANASUMBULIWA NA MARADHI YA  KISUKARI NA BP KWA MUDA MREFU. MAREHEMU ALICHUKUA CHUMBA TAREHE 10.04.2014 MAJIRA YA  SAA 16:00 JIONI  NA ALIFANYA KITENDO HICHO BAADA YA   KUJIFUNGIA KWA NDANI KATIKA CHUMBA NAMBA 13 KISHA KUJIUA NA KISU. KISU ALICHOKITUMIA KIJIUA KILIKUTWA BADO KIPO SHINGONI.  AIDHA MAREHEMU HAKUACHA UJUMBE WOWOTE. MWILI WAKE ULIKUTWA NDANI KATIKA BAADA YA ASKARI POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WENYE NYUMBA KUVUNJA MLANGO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI INA MADHARA KWA JAMII.




Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »