MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI HUKU MFANYABIASHARA MMOJA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KICHWANI NA WATU WASIOFAHAMIKA.



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 17.04.2014.

·         MFANYABIASHARA MMOJA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KICHWANI NA WATU WASIOFAHAMIKA.

·         MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.

·         WATU WATANO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PETTER MWAMBENE (38) MFANYABIASHARA YA KUBADILISHA FEDHA KIENYEJI, MKAZI WA KALOLENI – TUNDUMA WILAYA YA MOMBA ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KICHWANI NA KISOGONI NA WATU WASIOFAHAMIKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA HUKO KATIKA MTAA WA KALOLENI, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA MNAMO TAREHE 16.04.2014 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU. WATU HAO KABLA YA KUFANYA TUKIO HILO WALIMVIZIA MAREHEMU NJIANI KATIKA UCHOCHORO WAKATI ANARUDI NYUMBANI AKIWA UMBALI WA MITA CHACHE KABLA YA KUFIKA KWAKE NA KUMVAMIA KISHA KUMSHAMBULIA. AIDHA INADAIWA KUWA MAREHEMU BAADA YA KUPEKULIWA KATIKA MIFUKO YAKE ALIKUTWA NA KIASI CHA FEDHA DOLA ZA KIMAREKANI 1,460.

MSAKO MKALI UNAFANYWA NA ASKARI WA TUNDUMA – TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA NAKONDE – ZAMBIA ILI KUWABAINI NA KUWAKAMATA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILO AZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE/WAKAMATWE  NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

KATIKA TUKIO LA PILI:

MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO KATIKA SHULE YA MSINGI IKUTI JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HAPPY SAMSON (12) AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.766 ADJ AINA YA TOYOTA LAND CRUISER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA EDWARD MOSES.

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 16.04.2014 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO KATIKA ENEO LA IYUNGA, KATA NA TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA, GARI LIPO KITUONI.

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA WITO MADEREVA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUVUKA SEHEMU YENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING] ILI KUEPUKA AJALI.

KATIKA MISAKO:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO 1. HURUMA LWANJI (27) MFANYABIASHARA 2. BETTY EVOD (19) 3. YOHANA BENEDICTO (27) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA MWAOGA 4. NEEMA MWANDOLELA (26) NA 5. PATRICIA MWANDANJI (35) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA MAMBA WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI 1. RIDDER PAKETI 139, DOUBLE PUNCH PAKETI 42, CHARGER PAKETI 02 NA BOSS WHISKY PAKETI 31.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOENDESHWA NA JESHI LA POLISI MNAMO TAREHE 16.04.2014 MAJIRA YA KUANZIA SAA 17:30 HADI SAA 18:15 JIONI HUKO KATIKA VIJIJI VYA MWAOGA NA MAMBA, KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA MARA MOJA KUJIHUSISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BIDHAA HIZO ILI WAKAMATWE NA HATUA KALI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.



Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »