Mtu mmoja amenusurika kifo kwa kujinusuru katika kichaka katikati ya maji yanayokwenda kasi akisubiri kuokolewa katika eneo la ruvu mkoani Pwani baada ya kuzidiwa nguvu na maji alipojitosa kwenye maji kwa nia ya kutafuta baiskeli yake huku hali ya usafiri ikitarajiwa kurejea katika hali yake ya kwaiada baada ya maji kupungua huku wakandarasi kutoka Tanroad wakihangaika kutengeneza maeneo yaliyoharibiwa na mvua.
Wakisumulia tukio hilo mashuhuda wameiambia TV kuwa mtu huyo alijitosa mwenyewe kwenye maji kwa nia ya kutafuta baiskeli yake aliyodai imesombwa na maji na kisha kuzidiwa nguvu na kasi ya maji katika eneo hilo na kisha kunasa katika kichaka akisubiri kuokolewa huku baadhi ya mashuhuda wakiwa kando wasijue la kufanya kumnusuru.
EmoticonEmoticon