MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KATIKA SHIMO LENYE MAJI




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 07.04.2014

·         MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KATIKA SHIMO LENYE MAJI.

·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA BHANGI.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NANDANGA KIDATO CHA KWANZA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUKAS MSUKWA (16) ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KATIKA SHIMO LA MAJI LILILOCHIMBWA NA WATENGENEZA BARABARA YA MPEMBA HADI WILAYANI ILEJE.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 05.04.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA NANDANGA, WILAYA YA MOMBA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI BAADA YA MAREHEMU KUTELEZA NA KUTUMBUKIA KATIKA SHIMO HILO LENYE UREFU WA KINA KATI YA FUTI 20 NA ZAIDI AMBALO LILIKUWA NA MAJI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUFUKIA MASHIMO YALIYO WAZI BAADA YA KUTUMIKA KWANI NI HATARI KWA WATOTO NA HATA WATU WAZIMU. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO HASA WALE WANAOISHI JIRANI NA MITO/MABWAWA KUTOWARUHUSU KUSOGELEA MAENEO YENYE MAJI KWANI NI HATARI KWA MAISHA YAO.



TAARIFA YA MSAKO:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FESTO SALILE (39) MKAZI WA MBUGANI AKIWA NA BHANGI KETE 10 SAWA NA UZITO WA GRAMU 50.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 05.04.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MALEZA, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMAI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.





Previous
Next Post »