Wezi wa mifugo weanaoshukiwa kuwa Wafulani wamewaua watu 79 katika kijiji kimoja Kaskazini mwa Nigeria katika jimbo la Zamfara.
Vyombo vya habari nchini Nigeria mnamo Jumapili vilimtaja Msemaji wa Gavana wa jimbo hilo, Bwana Nuhu Salihu Anka, akisema kuwa watu hao waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wezi wa mifugo kutoka jamii ya Fulani, ambao ni wachungaji.
Maafisa wakuu katika Serikali ya jimbo la Zamfara walihudhuria mazishi ya watu hao 79 katika eneo hilo hiyo jana. Naye msemaji wa polisi wa Taifa, Lawal Abdullahi alisema kuwa watu 30 waliuawa katika shambulio la Jumamosi wakati wachungaji waliokuwa na bunduki kutoka jamii ya Fulani walipovamia mkutano wa wajumbe kutoka Majimbo ya Zamfara, Kaduna, Kebbi na Kastine wakijadiliana changa moto za usalama katika maeneo yao.
Anka anatajwa kusema kwamba wamekuwa wakikabiliana na mashambulizi mabaya sana ya magenge ya watu wenye silaha na wezi wa ngombe lakini shambulio hili la sasa ndiyo baya zaidi.
Kiongozi mmoja wa kijadi amenukuliwa akisema idadi ya waliokufa ni wengi zaidi. Alisema hadi kufikia Jumapili walikuwa wamewazika watu 120 kutokana na shambulizi hilo na kuwa idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka zaidi.
Artikel Menarik Lainnya
Rais Magufuli Asema Hatagawa Chakula cha Bure Kwa Watakaopatwa na Janga la Njaa Bila Sababu za Msingi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali
WAZIRI MKUU AWAPONGEZA MADAKTARI WA TAASISI YA KIISLAM YA BILAL WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewashukuru na kuwapongeza madaktari wa Taasisi ya Bilal Muslim
SABODO AMSHAURI RAIS MAGUFULI AZIDI KUPUNGUZA BARAZA LA MAWAZIRI Mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo akizungumza nyumbani kwake Upanga Dar es Sa
JUMUIYA YA WATANZANIA WANAOSOMA BEIJING WAADHIMISHA MIAKA 53 YA MUUNGANO Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania wanaosoma Beijing Nchini Husein Mtoro ( katik
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella Asema Hakuna UGAIDI Jijini Mwanza Wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza likiwashikilia watu 14 kwa tuhuma za mauaji ya wat
KIFAHAMU KIPINDI KIPYA CHA 'CHUKUA HATUA' KINACHOHUSU VIJANA MKOANI DODOMA Watangazaji wa kipindi kipya cha CHUKUA HATUA Happy Balisidya na Mohammed Hammie, siku
EmoticonEmoticon