TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 28.04.2014.
·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WATU
WASIOFAHAMIKA KWA TUHUMA ZA WIZI.
·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE WANNE
KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA BARABARANI.
·
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MIWILI AFARIKI DUNIA
BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE DIBWI LA MAJI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAKARI IBRAHIM
(22) MKAZI WA CHIMALA WILAYA YA MBARALI ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA NA
KITU KIZITO KICHWANI KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO LIMETOKEA
MNAMO TAREHE 27.04.2014 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI
CHA SIMIKE - CHIMALA, KATA YA
CHIMALA, TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA
MBARALI MKOA WA MBEYA, KANDO KANDO YA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. INADAIWA
KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU KUIBA TV MOJA PAMOJA NA REMOTE
TATU ZILIZOKUTWA KANDO YA MWILI WAKE AMBAZO MMILIKI BADO KUFAHAMIKA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA
VYOMBO HUSIKA KWA TARATIBU ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
GARI LENYE NAMBA
ZA USAJILI T.773 BEY AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA
NA DEREVA NGAMILE AFWILILE (36)
MKAZI WA MBEYA LILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI AITWAYE LWITIKO AMBAKISYE (37) MKAZI WA KIWIRA WILAYANI RUNGWE ALIYEKUWA
AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.607
BEM AINA YA SHANREY NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
PAPO HAPO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.04.2014
MAJIRA YA SAA 20:45 USIKU HUKO
KATIKA ENEO LA SOGEA-TUKUYU, KATA YA TUKUYU, TARAFA YA UKUKWE, BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE
MKOA WA MBEYA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WANNE WALIJERUHIWA AMBAO NI 1.
BARAKA SANTE (35) MKAZI WA MWANJELWA 2.
LUGANO ALAMU (28) MKAZI WA KK-TUKUYU 3.
MTOTO SHAFII BARAKA (7) MKAZI WA TUKUYU NA 4. DEVOTA NJOLE (25) MKAZI WA KK-TUKUYU AMBAO WAMELAZWA HOSPITALI
YA MAKANDANA –TUKUYU.
CHANZO CHA AJALI
NI MWENDO KASI WA GARI NA MWILI MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MAKANDAMA –
TUKUYU, DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI
(DEREVA) AZITO KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTOTO MWENYE
UMRI WA MIAKA MIWILI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GEOFREY AMANI, MKAZI WA KAFUNDO WILAYANI KYELA AMEFARIKI DUNIA
BAADA YA KUTUMBUKIA KATIKA DIBWI LA MAJI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.04.2014
MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAFUNDO,
KATA YA IPINDA, TARAFA YA NTEBELA, WILAYA YA KYELA. INADAIWA KUWA MTOTO HUYO
ALIKUWA ANACHEZA KWENYE MADIBWI YA MAJI YALIYOPO JIRANI NA NYUMBA YAO HALI
ILIYOPELEKEA KUTUMBUKIA KATIKA MOJA YA MADIBWI HAYO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI
KUWA MAKINI KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WADOGO HASA KATIKA
KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA
JITOKEZA. AIDHA NI VYEMA KUFUNIKA VISIMA NA KUFUKIA MADIBWI YA MAJI KWNI NI
HATARI KWA WATOTO.
KATIKA MSAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AKWINO MARTIN (28) MKAZI WA KIJIJI CHA ISANGAWANA WILAYANI CHUNYA AKIWA ANAMILIKI
SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA NUSU HEKTA.
MTUHUMIWA HUYO
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.04.2014
MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MAZIMBO, KATA YA MATWIGA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA,
MKOA WA MBEYA. BHANGI HIYO IMEHARIBIWA NA ILIKUWA NA UREFU WA FUTI NNE [04]. MTUHUMIWA NI MKULIMA/MTUMIAJI
NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUJIHUSISHA NA ULIMAJI WA ZAO HARAMU LA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon