TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 27.04.2014.
·
MTOTO WA MIAKA MITATU AUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA
BABA YAKE MZAZI.
MTOTO WA MIAKA MINNE AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUGONGWA NA GARI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VANESA PATRICK
NJOJO (03) MKAZI WA ISISI, WILAYANI
MBARALI ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI AITWAYE PATRICK
NJOJO (23) MKAZI WA
ISISI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014
MAJIRA YA SAA 23:45 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISISI, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA
MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI ULEVI WA POMBE ZA KIENYEJI WA BABA
HUYO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA
WILAYA MBARALI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUEPUKA ULEVI KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA UNA MADHARA KATIKA JAMII. AIDHA
ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWAFUNDISHA WATOTO WAO KWA UTARATIBU MZURI ILI
KUEPUKA MATATIZO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO MWENYE
UMRI WA MIAKA 4 – 5 ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA FESTO MBIGA, MKAZI WA NSALAGA AMEFARIKI DUNIA
PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI SM 9124 AINA YA FAW LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA RAMADHANI
MWALYOYO (30) MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014
MAJIRA YA SAA 14:45 MCHANA HUKO
KATIKA KIJIJI CHA NSALAGA, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA, BARABARA KUU YA
MBEYA/IRINGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon