MLINZI WA KAMPUNI BINAFSI YA ULINZI AUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA.





TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 08.04.2014.


·         MLINZI WA KAMPUNI BINAFSI YA ULINZI AUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA.

·         MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MLINZI MMOJA WA KAMPUNI BINAFSI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HAMISI RAMADHAN (50) MKAZI WA SOGEA ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI WEZI AKIWA KAZINI.

TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 02:15 HUKO KATIKA ENEO LA MSIKITINI TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, WATU HAO KABLA YA KUTEKELEZA MAUAJI HAYO, WALIMVIZIA MHANGA WAKATI AMEKAA KWENYE VARANDA MOJA WAPO KATI YA  MADUKA MAWILI ANAYOLINDA AKIOTA MOTO NA KUMPIGA. AIDHA WATU HAO WALIVUNJA MADUKA MAWILI [DUKA LA DAWA NA DUKA LA FURNITURE] KWA LENGO LA KUIBA LAKINI HAWAKUFANIKIWA KUCHUKUA KITU CHOCHOTE KWANI WALINZI WA MADUKA JIRANI WALITOA TAARIFA KWA ASKARI WA DORIA AMBAO WALIANZA KUWAKIMBIZA WEZI HAO NA KUELEKEA CHIANGA –NAKONDE ZAMBIA.

MSAKO MKALI UNAENDELEA KWA USHIRIKIANO KATI YA POLISI WA TUNDUMA NA NAKONDE ILI KUWAKAMATA WATUHUMIWA HAO AMBAO WAMETOKEA ENEO HILO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.3

KATIKA TUKIO LA PILI:

MTEMBEA KWA MIGUU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LAMECK LUSAMBO (31) MKAZI WA IGAWA AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI STK 6915 AINA YA TOYOTA LAND CRUISER MALI YA  WIZARA YA  NISHATI NA MADINI LILIKUWA LIKITOKEA MKOA WA NJOMBE KUELEKEA MBEYA MJINI LIKIENDESHWA NA DEREVA BALTAZAL NYAMBITI (45) MKAZI WA DSM.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 07.04.2014 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA IGAWA KATA YA LUGELELE, TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA, BARABARA KUU YA MBEYA /NJOMBE. INAELEZWA KUWA CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO CHA POLISI RUJEWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

Signed by:
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »