MAMA ALEWA NA KUMLALIA MWANAWE HADI KUFA, MWINGINE AMUUA BABA YAKE KWA JEMBE



Mama alewa na kumlalia mwanae hadi kumuua; mwingine amuua baba yake kwa jembe
WATU wawili wamekufa Mkoani Kilimanjaro, katika matukio mawili tofauti, likiwemo la mtoto kufariki dunia baada ya kuangukiwa na mama yake mzazi aliyekuwa amelewa pombe.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro,Robert Boaz, ameiambia FikraPevu leo Jumatatu Aprili 7, 2014 kwamba tukio hilo lilitokea saa 4.30 usiku wa jana katika kijiji cha Mkoshao Mkomilo Wilaya ya Moshi, baada ya Theresia Boniphace (30), akiwa amelewa kumwangukia hadi kumuua mwanae mchanga mwenye umri wa  miezi mitano Agripina Boniphace.
Amesema mama mzazi huyo alirejea nyumbani usiku huo kutoka katika kumbi za starehe na alipopewa kichanga hicho na mfanyakazi wa ndani kwa lengo la kumnyonyesha, lakini kabla ya kumnyonyesha alianguka naye na kusababisha kifo chake papo hapo.

"Chanzo cha tukio hili ni ulevi wa kupindukia, kwani inaelezwa kuwa Mama huyu baada ya kurudi nyumbani alikabidhiwa mwanaye kwa ajili ya kumnyonyesha,na ndipo alipoanguka naye na kumlalia na kusababisha kifo chake" alisema Kamanda Boaz.

Amesema mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya (KCMC) na kwamba Mama huyo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

Amuua Baba yake kwa kumshambulia  ‘jembe’

Katika tukio la pili mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Stephen Maro(65), mkazi wa Uru Mawela, amekufa baada ya kushambuliwa na mwanae katika sehemu mbalimbali za mwili wake kwa jembe lenye ncha kali maarufu kama rato.

Ameiambia  kuwa tukio hilo lilitokea Jumapili Aprili 6, mwaka huu, majira ya saa 4:45 asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya (KCMC) mahali ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.

Kamanda Boaz, alisema marehemu alipigwa kwa Rato kichwani, Shingoni nakuvunjwa mkono wake wa kulia mara mbili na mwanae aitwae Thomas Stephen (33), ambapo kijana huyo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi na pindi utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake huku akisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitalia ya (KCMC).
Previous
Next Post »