Katibu wa Taasisi na Jumuiya ya Waislamu Tanzania , Sheikhe Ponda Issa Ponda ( mwenye kanzu) akisindikizwa na baadhi ya Askari Kanzu na wakawaida |
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Morogoro kwa mara nyingine leo imeshindwa kuanza kusikiliza kesi ya Katibu wa Taasisi na Jumuiya ya Waislamu Tanzania , Shehe Ponda Issa Ponda kutokana na jadala halisi kutorejeshwa kwenye Mahakama hiyo toka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam na hivyo kuiahirisha hadi Mei 14, mwaka huu.
Katibu wa Taasisi na Jumuiya ya Waislamu Tanzania , Sheikhe Ponda Issa Ponda ( mwenye kanzu) akiwa ndani ya chumba cha Mahakama akisubiri hatima ya kesi yake |
Katibu wa Taasisi na Jumuiya ya Waislamu Tanzania , Sheikhe Ponda Issa Ponda ( mwenye kanzu) akisindikizwa na baadhi ya Askari Kanzu na wakawaida , kutoka Mahakamani |
Baadhi ya wafuasi wa Katibu wa Taasisi na Jumuiya ya Waislamu Tanzania , Sheikhe Ponda Issa Ponda wakitoka kwenye viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro |
Shehe Ponda alifikishwa Mahakamani hapa majira ya saa tatu asubuhi chini ya Ulinzi mkali wa Polisi ,ambapo pia baadhi ya wafuasi wake walifika mapema Mahakamani hapo wakitakiwa kubakia nje ya uzio .
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mkoa , Mary Moyo , anayesikiliza kesi hiyo alitumia dakika tatu kufikia kutoa maamuzi kuahirisha kutokana na Jadala halisi la kesi kuendelea kubakia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Aliufahamisha upande wa wakili wa serikali na Wautetezi kuwa hakuwa na jalada halisi la kesi hiyo na bado haijarejeshewa toka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, lilipopelekwa kwa ajili ya kusikilizwa ombi la Sheikhe Ponda la mapitio lililowasilishwa kwenye Mahakama kuu hiyo siku za nyuma.
Sheikhe Ponda amefuguliwa kesi namba 128/2013 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro akikabiliwa na Mashitaka matatu ambayo aliyatenda Augosti 10, 2013, eneo la Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro na alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Augosti 19, 2013.
EmoticonEmoticon