Kijana Mmoja aliyetuhumiwa kuwa Kibaka Akiwa amekaa kwa Huruma mara baada ya Kushushiwa Kipigo na wanaodhaniwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe cha Mjini Morogoro ..Wanafunzi wa Chuo Kukuu Mzumbe walimkamata Kijana Mmoja anayesadikiwa kuwa kibaka kwenye moja ya Mabweni yao akijaribu kuiba vitu mbali mbali na Ndipo walipomshushia kichapo hadi kinachodaiwa kupoteza maisha
Kibaka huyo akiwa amelala chini mara baada ya Kupigwa
Tukio hilo lilitokea saa nane usiku ambapo kibaka huyo anayeisha nje ya Chuo hicho alikamatwa na mmoja wa wanafunzi ndani ya Bweni akiwa na lundo la Nguo na viatu.Shuhuda wa alisema Kwa muda mrefu wanafunzi hao walilalamika kuibiwa vitu vyao na watu wasiowafahamu.
Kibaka huyo aligoma kutua mizigo hiyo jambo linalodiwa kuzidisha hasira kwa Wanafunzi hao na kuzidisha kumshambulia.
Baada ya kukithiri kwa vitendo hivyo Chuoni hapo Wanafunzi waliamua kuongeza umakini wa kubaini mwizi wao ambapo mmoja wa wanafunzi ambaye alikuwa akijisome alisikia kishindo cha mtu kwenye Korido la Bweni lake ambapo baada ya kuchungulia alimshuhudia kibaka huyo akitoka na vitu mbali mbali ndipo alipoamua kupiga mayowe ya Mwizi yaliowaamusha wenzake ambao walimzingira kibaka huyo na kumkamata akiwa na kithibiti mkonono
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
EmoticonEmoticon