Rais Uhuru Kenyatta, atapunguziwa mshahara wake kwa Sh 248,000 za Kenya karibu sawa na dola 3,000, na naibu rais William Ruto anapunguziwa Sh210,000. mawaziri na makatibu wakuu wote wanapunguziwa pia mishahara yao kwa asili mia 10.
Rais Kenyatta alitangaza uwamuzi huo siku ya Alhamisi baada ya mkutano na maafisa wa juu wa serikali na wajumbe wa kamati ya bajeti ya bunge mjini Nyanyuki, na kueleza kwamba serikali hivi sasa inatafakari na kujadili kupunguza matumizi ya safari za kigeni katika lengo la kupunguza matumizi na kuweza kupata fedha kutumika kwa miradi ya maendeleo.
Akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano huo, Rais Kenyatta alisema serikali inatafakari pia juu ya kufutilioa mbali matumizi ya umaa mabayo hayaleti faidi au kuimarisha maisha ya wakenya.
Wachambuzi wa kisiasa wanasema uwamuzi huo wa kihistoria unaonekana umechukuliwa kwa lengo la kuanzisha mjadala wa kitaifa juu ya kupanga upya mishahara ya watumishi wa serikali na matumizi, juhudi zinazoongozwa na Tume ya Mishahara na Matumizi, inayojaribu kupunguza bajeti ya mishahara ambayo inafikia $ bilioni 5 kwa mwaka.
Siku ya Jumatatu tume hiyo itakua na mjadala wa umaa juu ya mswada wa mishahara ya serikali katika ukumbi wa jengo mikutano ya kimataifa ya Kenyata KCC mjini Nairobi.
CREDIT: VOA SWAHILI
EmoticonEmoticon