Ngozi Kavu inahitaji uangalizi wa hali ya juu sana kwa sababu ngozi hii huwa inakibiliwa sana na mikunjo na chunusi. Hali hii hutokea hasa kipindi cha baridi ambapo ngozi huwa inakua kavu. Lakini kuna vitu unavyoweza kufanya ili kuweza kuitunza ngozi kwa kupunguza ukavu na wakati huo huo ukiipa ulinzi dhidi ya kuzeeka mapema kwa ngozi.
- Osha uso wako kila siku na sabuni ya kusafishia uso ambayo haina kemikali na kamwe usitumie sabuni ambayo itaondoa asili ya mafuta kwenye ngozi yako.
- Tumia vilainishaji ngozi kila siku wakati wa mchana na unapopaka kilainishi kwenye ngozi yako, chua ngozi yako kwa mduara kwa kwenda juu na sio kuvuta au kusugua ngozi yako.
- Paka cream kwenye ngozi yako kabla ya kwenda kulala. Ni vyema kutumia cream ambazo zina Alpha Hydroxy Acids au AHA ambazo zinatengenezwa kwa kutumia michanganyiko inayojulikana kama vile maziwa, matunda na sukari. Alpha Hydroxy Acids hukausha, huua na kuondoa tabaka la ngozi ya nje huku ikilainisha ngozi mpya inayotoka.
- Kama ngozi yako ni kavu na inaelekea kuwa nyekundu yenye mistari inayouma au vipele unatakiwa kumuona daktari wa ngozi. Hali hii pia inaweza kusababishwa na hali ya hewa au vitambaa kama vile pamba, vitu tunavyopaka kwa ajili ya kutunza ngozi, sabuni na kadhalika.
Daktari anaweza kukushauri ni cream gani utumie kulainisha ngozi yako na kuondoa wekundu kwenye ngozi yako pia kuondoa bugudha kwenye ngozi yako kama vile kutumia vitambaa vya cotton na kuepuka watu wengi wanapata matatizo kuwa na ya ngozi kavu hasa kutokana na hali ya hewa. Kama ni miezi ya baridi husababisha ngozi yako kuwa kavu, matumizi ya mara kwa mara ya vilainishi vitasaidia ngozi yako kuwa ngavu na nyororo.
EmoticonEmoticon