Pichani ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani.
Na Edwin Moshi, Njombe
Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Bw. Yusufu Sadick Mkalile (33) kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaaa mwenyewe kwa kumziba pua na mdomo
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani imesema kuwa mtuhumiwa alitenda mauaji hayo Machi 16 mwaka huu majira ya saa 03:20 asubuhi, ambapo alimziba pua na mdomo mwanaye huyo aitwaye Udai Yusufu (8) hali iliyosababisha kukosa hewa na kufariki
Tukio hilo limetokea chumbani, nyumbani kwao mtaa wa Nazareth, kata ya Mjimwema tarafa ya Njombe Mjini wilaya ya Njombe, na hadi anafariki marehemu alikuwa akisoma darasa la pili katika shule ya Msingi Meta mkoani Mbeya
Mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni mkulima mkazi wa Stereo mkoani Mbeya amekamatwa na polisi na anaendelea kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo na chanzo bado hakijafahamika.
EmoticonEmoticon