WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI
KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 04.01.2014 MAJIRA YA SAA 10:55HRS HUKO MAENEO YA MLIMA NYOKA, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA,
BARABARA YA MBEYA/IRINGA. GARI T.437 AQW AINA YA TOYOTA COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA
ANUANI YAKE LILIMGONGA MPANDA BAISKELI AITWAYE ASHURA D/O MWINUKA, MIAKA 22, MKINGA, MKAZI WA UYOLE NA KUSABABISHA
KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI
NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA
SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI
AZITOE ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE
MWENYEWE.
WILAYA YA RUNGWE –
KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 04.01.2014 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO MTAA WA IGOGWE TUKUYU MJINI, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA,
ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO
WALIMKAMATA RAYMOND S/O EMMANUEL,
MIAKA 27, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIWIRA ROAD TUKUYU MJINI AKIWA NA BHANGI KETE 364 NA MISOKOTO 10 SAWA NA UZITO
WA KILO 01 NA GRAM 820. BHANGI HIYO ALIIFICHA KATIKA MIFUKO YA RAMBO. MTUHUMIWA
NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA
NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUWAFICHUA WATU
WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE.
[AHMED. Z. MSANGI –
SACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon