WILAYA
YA MBEYA VIJIJINI – UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA [PANGA].
v
MNAMO
TAREHE 03.01.2014 MAJIRA YA SAA 17:35HRS HUKO ENEO LA MLIMA KAWETELE BARABARA YA MBEYA/CHUNYA KATA YA LWANJILO TARAFA YA TEMBELA WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI MKOA WA MBEYA. SREEDHAR S/O PASUPELETI, MIAKA 38,
HINDU, MFANYABIASHARA MWENYE ASILI YA KIHINDI, MKAZI WA MAKATA – CHUNYA AKIWA
KATIKA GARI T.756 ABL AINA YA TOYOTA
PICK UP NA WENZAKE WAWILI ALINYANG’ANYWA PESA TSHS 3,700,000/= NA WATU
WATANO WALIOKUWA NA GARI NDOGO T.782 BEU AINA YA GX 100 T/CRESTA NA GARI LINGINE LISILOKUWA
NA NAMBA ZA USAJILI LENYE NAMBA ZA
CHASES GX - 6011835 AINA YA GRAND MARK II.
v
MBINU NI KUVIZIWA NJIANI WAKATI WAKIELEKEA CHUNYA KUTOKA MBEYA MJINI NA
WATU HAO AMBAO WALIWEKA MAGOGO
BARABARANI NA KUDAI GARI LAO NI BOVU KISHA KUWAPORA WAHANGA PESA HIZO PAMOJA NA
BEGI LILILOKUWA NA NGUO NA VITU MBALIMBALI KWA KUWATISHIA KWA KUTUMIA SILAHA
AINA YA MAPANGA.
v
WATUHUMIWA WATANO WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO
HILI 1.B.500 SGT JUMA S/O MUSA, MIAKA
38, MMANYEMA, ASKARI MAGEREZA WA GEREZA LA RUANDA MBEYA 2. F.8302
PC JAMES, MIAKA 32, MUHA, ASKARI POLISI WILAYA YA MBEYA 3. MBARUKU S/O HAMISI, MIAKA 29, MUHA, MKAZI
WA FOREST 4. AMRI S/O KIHENYA, MIAKA
38, MKAZI WA FOREST NA 5. ELINANZI S/O
MSHANA, MIAKA 29, MPARE, MKAZI WA FOREST.
v
WATUHUMIWA HAO WALIKUTWA NA BAADHI YA MALI
WALIZOPORA AMBAZO NI MABEGI MATATU YA NGUO, SIMU MOJA YA KIGANJANI AINA YA
SAMSUNG NA LAPTOP MOJA AINA YA
SAMSUNG VILIVYOKUTWA KWENYE GARI GX
- 6011835 AINA YA GRAND MARK II
NA MABLANKETI MAWILI YALIYOKUTWA KWENYE BUTI LA
GARI T.782 BEU AINA YA GX 100 T/CRESTA.
v
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUJIEPUSHA NA TAMAA ZA MALI NA KUJIPATIA
UTAJIRI WA HARAKA KWA NJIA ZISIZO HALALI NA BADALA YAKE WAFANYE SHUGHULI ZILIZO
HALALI ILI WAJIPATIE KIPATO.
WILAYA
YA MBEYA MJINI – AJALI YA MOTO.
MNAMO TAREHE 03.01.2014 MAJIRA YA SAA
21:00HRS HUKO ENEO LA FOREST KATA
YA FOREST, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. EMANUEL S/O JANCO, MIAKA 48, MCHAGA, MFANYABIASHARA ,MKAZI WA
FOREST ALIGUNDUA KUUNGUA MOTO KWA VYUMBA VITATU VILIVYOPO KATIKA MOJA KATI YA
JENGO LA HOTELI YAKE NA KUSABABISHA VITU MBALIMBALI KUTEKETEA KWA
KUUNGUA MOTO. CHANZO KINACHUNGUZWA.
HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. THAMANI HALISI YA MALI
ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA. MOTO HUO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA KIKOSI
CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI, ASKARI POLISI NA WANANCHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUCHUKUA TAHADHARI NA MAJANGA YATOKANAYO NA MOTO ILI KUJIEPUSHA NA
MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI – AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
MNAMO TAREHE 03.01.2014 MAJIRA YA SAA
15:45HRS HUKO ENEO LA HOSPITALI TEULE YA IFISI WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI MKOA WA MBEYA KATA YA SONGWE, TARAFA YA BONDE LA SONGWE. GARI T.330 ACK/T.422 ACK AINA YA SCANIA
SEMI TRAILLER TANKER LIKIENDESHWA NA
DEREVA YUSU S/O SULEIMAN FAKHI, MIAKA 45, MKAZI WA MAGOMENI DSM,LIKITOKEA MBEYA KUELEKEA TUNDUMA LILIGONGANA NA GARI T.897 ALH AINA YA TOYOTA HAICE ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA
DEREVA MUSA S/O HAMIS, MIAKA 25, MLUGURU, MKAZI WA IYUNGA LILILOKUWA
LIKITOKEA TUNDUMA KUJA MBEYA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO AMBAYE BADO
HAJAFAHAMIKA JINA WALA MZAZI WAKE MWENYE UMRI WA MIEZI KUMI [10] JINSI YA KIKE NA MAJERUHI KWA ABIRIA 13 KATI YAO WANAWAKE
TISA NA WANAUME WANNE WAKIWEMO WATOTO WADOGO WAKIKE WAWILI NA WAKIUME MMOJA. MAJERUHI WAWILI
WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA MAJERUHI 11 WAMELAZWA HOSPITALI TEULE YA
IFISI AKIWEMO DEREVA WA GARI T/HAICE NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA
WA GARI T.330 ACK/T.422 ACK
AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED. Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA
YA MBARALI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 03.01.2014 MAJIRA YA SAA
12:12HRS HUKO IGURUSI – KITUO CHA
MABASI, KATA YA IGURUSI, TARAFA
YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA MAWAZO S/O JIMU, MIAKA 32, MBENA NA MKAZI WA
ILOLO IGURUSI AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 14
SAWA NA UZITO WA GRAM 70. MTUHUMIWA
NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa
na:
[AHMED.
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon