TAARIFA YA UFAFANUZI KUTOKA KWA WAZIRI MKUU NI KWAMBA MHESHIMIWA RAIS KIKWETE AMERIDHIA KUTENGA UTEUZI WA MAWAZIRI WANNE


Waziri  mkuu  wa Jamhuri ya  muungano  wa Tanzania  Mizengo  Pinda amesema kuwa amesikiliza kwa makini  vitendo  vya unyanyasaji  ambavyo  vimefanywa na kikosi  cha kupambana na ujangili katika hifadhi maarufu kama TASK FORCE.

Alisema  kuwa lengo la serikali kuunda  kikosi  hicho ilikuwa ni kupambana na ujangili  ila tatizo  limekuja katika usimamizi  wa suala  hilo.

Hivyo amesema  kuwa anakubaliana na mawazo ya  wabunge  dhidi ya  mawaziri  hao  ili  kuchukua hatua  kutokana na mazingira ya hayo  yaliyozungumzwa.

Pinda  alisema  kuwa anaungana na mwanasheria  wa serikali  kuwa muda wa kamati  hiyo  ulikuwa ni mdogo  hivyo ni  vema  kuendelea  zaidi  ili  hatua  stahiki  kuchukuliwa kwa  wahusika.

" Hapa  ninaona  kuna upungufu  mkubwa wa  mapungufu  ya kisheria  hivyo ni vema kuwapa  watu ambao  wana haiba ya  kufanya kazi  hiyo ili  kutumia muda japo  wa mwezi  mmoja ili kuchukua hatua"

Alisema kuwa  baada ya kupokea  maoni ya  wabunge  yeye kama  waziri  mkuu alipata  kukutana na  mawaziri  wanne  waliotajwa na  kuwashauri  kuchukua hatua.

Mawaziri  hao  ni waziri wa maliasili na utalii, waziri  wa jeshi la kujenga  Taifa Shamsi Vuai Nahodha,waziri  wa mambo ya ndani  Dk Emmanuel Nchimbi, na waziri  wa mifugo  Mathayo David ambao kila mmoja amejieleza  yake.

Alisema  kuwa kwa upande wa waziri David Mathayo  amepata  kujieleza ni namna gani anapaswa  kuwajibika kwa oparesheni tokomeza ama hapaswi  kujiuzulu.

Pia  alisema amepata  kuzungumza na Rais  Dr  Jakaya  Kikwete na yeye ameunga mkono mawazo  ya  wabunge na kutaka watendaji  ambao wamehusika wachukuliwe  hatu .

Pia alisema kuwa Rais Kikwete amekubali  kutengua  uteuzi  wa mawaziri wote wanne  akiwemo waziri Mathayo 
Previous
Next Post »