TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI“PRESS RELEASE” TAREHE 20.12. 2013.



WILAYA YA MOMBA – MAUAJI.

MNAMO TAREHE 19.12.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA TAZARA -TUNDUMA   KATA NA TARAFA YA TUNDUMA   WILAYA YA  MOMBA  MKOA WA MBEYA. MTOTO KALIBU S/O KIMWELU, MIAKA 6, MNYAMWANGA,  MKAZI WA MTAA WA TAZARA TUNDUMA ALIUAWA KWA KUCHINJWA SHINGONI KWA KUTUMIA  KISU   NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. AIDHA WATU HAO WALIMNYONGA SISTA D/O NYILENDA, MIAKA 17, MNYIHA, MFANYAKAZI WA NDANI [HOUSE GIRL] KWA KUTUMIA WAYA WA TELEVISHENI ULIOKUWEPO SEBULENI. MBINU NI KUWAVAMIA WAHANGA WAKIWA NDANI NYUMBANI KISHA KUWAUA KINYAMA. MIILI YA MAREHEMU WOTE ILIKUTWA SEBULENI. WAKATI WA TUKIO BABA WA MTOTO AITWAE ESTON S/O KIMWELU,MIAKA 55, MNYAMWANGA,  DIWANI WA KATA YA  MKANGAMO - CCM,  MKAZI WA TAZARA  ALIKUWA  SHAMBANI KIJIJI CHA KIPAKA NA MAMA WA MTOTO AITWAE  TUMAINI D/O YOHANA, MIAKA 29, MNDALI, KATIBU MUHTASI  HALMASHAURI YA  MJI MDOGO WA TUNDUMA ALIKUWA KAZINI.  KATIKA TUKIO HILO WATU HAO PIA WALIIBA MABEGI MAKUBWA MAWILI YENYE NGUO MBALIMBALI YALIYOKUWA KATIKA CHUMBA WANACHOLALA WATOTO.  CHANZO KINACHUNGUZWA INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA NI MGOGORO WA MUDA MREFU WA  KIFAMILIA KATI YA  MKE MKUBWA NA MDOGO KUFUATIA FAMILIA YA  MKE MKUBWA KUDAI KUTELEKEZWA NA KUNYIMWA MALI/MASHAMBA.  WATUHUMIWA WATANO WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI AMBAO NI 1. GABRIEL S/O KIMWELU, MIAKA 19, MNYAMWANGA, MKULIMA 2. ENOCK S/O SIMWELU, MIAKA 23, MNYAMWANGA, MKULIMA 3. ALEX S/O SIMWELU, MIAKA 16, MNYAMWANGA, MWANAFUNZI KIDATO CHA PILI SHULE YA SEKONDARI MPAKANI WOTE NI WATOTO WA MKE MKUBWA, WAKAZI WA MAJENGO MAPYA TUNDUMA  4. MUSSA S/O NGOBA, MIAKA 19, MNYAMWANGA, MKULIMA MKAZI WA MTAA WA MWAKA – TUNDUMA NA 5. PATRICK S/O MSIGWA, MIAKA 18, MKINGA, MKULIMA MKAZI WA MAJENGO MAPYA TUNDUMA WOTE NI MAJIRANI NA MARAFIKI WA WATOTO HAO. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA KWA UCHUNGUZI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUZINGATIA SUALA LA MALEZI BORA KWA WATOTO NA VIJANA WAO ILI WAKUE KATIKA MAADILI MEMA NA KUJIEPUSHA NA MATUKIO YA UHALIFU. AIDHA ANASISITIZA ILI KUWA NA TAIFA LENYE USTAWI MZURI WA JAMII SUALA LA MALEZI BORA KWA WATOTO NI JUKUMU LETU SOTE. PIA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.






WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
                                                  NA KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 19.12.2013 MAJIRA YA SAA 21:00HRS HUKO ENEO LA STERIO KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA BARABARA YA SOKOMATOLA/MAFIATI  JIJI NA  MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI  LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU BOSCO S/O SANGANO, MIAKA 45, MMATENGO,  DAKTARI MWANAFUNZI HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI NA VYOMBO VYA MOTO ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTU ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE ZICHUKULIWE.



Signed by:
[B.N MASAKI – ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »