Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe Mbowe akizungumza mbele ya umati mkubwa wa wanachama na wapenzi wa chadema Mwanza jana
Katika kuzindua Mkoa wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu jijini Mwanza Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akizungumza na wanafunzi Goldcrest Hotel Mwanza
---
Katika kuzindua Mkoa wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu jijini Mwanza Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameeleza mambo mazito ambayo yanaweza kutafsiriwa kama somo kubwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, vijana na wanachama wa chadema kwa ujumla wake. Akihutubia mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika kiwanja kilichopo ofisi za Kanda ya Ziwa Magharibi eneo la Bwiru, mwenyekiti huyo wa CHADEMA ambaye pia ni mbunge wa Hai aliongea mambo kadhaa yaliyokuwa chini ya kichwa cha habari Historia ya CHADEMA.
CHADEMA imejengwa na watu kwa maumivu makubwa. Ndugu mbowe alitanabaisha kwamba kuna watu wamemwaga damu zao, kuna watu wamekuwa vilema,kuna watu wamefilisiwa na kuna watu wengine wamepoteza uhai wao kwa sababu ya kuanzisha na kukijenga chama cha CHADEMA. Katika kulifafanua hilo aliwachallenge vijana wa vyuo vikuu kama wanafahamu hata majina ya watu waliopoteza uhai wao au kuvurugiwa maisha yao kwa sababu ya CHADEMA. Akitoa mifano ya watu hao Mbowe alimtaja aliyekuwa balozi maalumu wa Tanzania UN ndugu Antoni Nyaki alivyovuliwa mara moja nafasi yake awamu ya mwinyi kwa kosa moja tu la kuwa mwenyeji wa Edwin Mtei alipokwenda Marekani katika harakati za kum-recruit Kabouru aliyekuwa huko Marekani kwa wakati huo. Pia Mbowe alimtaja ndugu Costa Shinganya kama victim aliyefilisiwa na kuamua kukimbilia Kongo kwa kosa la kusimama upande wa CHADEMA. Mifano mingine aliyotaja ni wafuasi wa CHADEMA kuuwawa katika maandamano, na mikutano kwa kurushiwa mabomu ya kivita kwa mfano pale Arusha.
Kuhusu elimu yake Mbowe ameeleza namna alivyofika Form 6 na kukwama kuendelea kutokana na mfumo wa elimu na ajira kwa wakati huo. Anasema alivyomaliza kidato cha sita alikwenda kufanya kazi BOT kabla ya kwenda chuo kwani kwa wakati huo mtu asingeweza kwenda chuo moja kwa moja bila kufanya kazi kwanza. Baada ya miaka mitano alipoomba kwenda chuo Governor wa BOT wa wakati huo Bob Makani marehemu hakumpa ruhusa ndipo alipoamua kuacha kazi na rasmi kuanza kujihusisha na mambo mengine ikiwemo siasa.
Historia ya CHADEMA, chama kilianza rasmi miaka ya tisini kipindi cha vuguvugu la uanzishwaji wa demokrasia ya vyama vingi.Ilipofika mwaka 1991 yeye na waasisi wengine 7 na baadae wakawa 14 wakaanzisha rasmi chama cha CHADEMA mkoani Dar-es-salaam kabla ya kukipeleka chama mikoani na visiwani Zanzibar. Akitaja majina ya waasisi wa CHADEMA,Mbowe alimtaja Edwin Mtei (mwenyekiti),Bob Makani (katibu mkuu), Costa Shinganya, Brown Ngwilupi, Edward Barongo(mwenezi), Mary Kabigi (kiongozi wanawake), Freeman Mbowe (Vijana), mama Marios (mwenyekiti wa kwanza Morogoro) Ndesamburo na wengine. Pia alidokeza kwamba mpaka uchaguzi wa mwaka 2000, CHADEMA haikuwahi kusimamisha mgombea wa uraisi.
Chanzo cha yeye kuwa mwenyekiti wa CHADEMA. Mbowe pia alisema kwa kipindi cha miaka ya 2000 hakuwa na wazo la kuwa mwenyekiti wala kugombea uraisi bali ni msukumo wa viongozi wa juu wa chama na vijana ndio uliochangia yeye kugombea nafasi hizo. Na yeye kwa kuheshimu hao viongozi aliafiki kuwa mwenyekiti lakini kwa masharti ya kupewa Dr. Slaa awe katibu mkuu wake na aruhusiwe kuanzisha reforms mbalimbali mdani ya chama, na huo ndio uliokuwa mwanzo wa uenyekiti wake.Akifafanua kwanini wenyeviti 2 wa mwanzo walijitoa mara baada ya awamu zao za kwanza tuu kuisha alibainisha kwamba umri wa wazee hao pia ulichangia.Alisema wote, Mtei na Bomani walianza uenyekiti wao wakiwa na miaka 60+ kwahiyo ilikuwa ni natural kwa wao kujitoa kwenye cheo hicho pengine kwa kuona wapumzike.
Onyo kuhusu "demokrasia". Mbowe pia alionyesha changamoto inayoweza kuletwa na dhana ya demokrasia kama busara haitatumika. Akitoa sababu za chama chake kutoweka wagombea uraisi hususani kwa mwaka 1995, Mbowe alisema kwanza ndugu mtei alichukua fomu ya kugombea uraisi, lakini siku chache kabla ya zoezi la kuchukua fomu halijasitishwa,kwa mshtuko, mzee Makani marehemu nae akachukua fomu hali iliyoleta mgawanyiko mkubwa ndani ya chama ukizingatia chama kilikuwa bado ni kichanga mno. Waliposhauriwa mmoja amwaachie mwingine,wote walikataa na hatimae kamati kuu ikaamua kuwaondoa wote na kutoweka mgombea katika kiti cha uraisi ili kukinusuru chama.Chanzo kikubwa kilikuwa ni demokrasia,kwamba kila mtu ana haki ya kugombea nafasi za uongozi chamani. Pia alifafanua umuhimu wa kufanya kazi ndani ya chama kama timu akitolea mfano wa LIonel Messi wa Barcelona namna alivyo tofauti na Lionel Messi wa Argentina sababu tu ya 'team work' na ugumu wa kucheza pekee yako kwenye ulingo wa siasa.
Mbowe na CHADEMA.Anasema akijua, na wanachama wenzake wakijua kwamba CHADEMA hawawezi kushinda mbio za uraisi mwaka 2005 wote hawakutaka kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huo.Hali hiyo pia ilichagizwa na mvuto wa kisiasa aliokuwa nao mgombea wa CCM kwa wakati huo, yaani Jk. Pamoja na hayo yote chama kilitambua umuhimu wa kumsimamisha mgombea wa uraisi ili kukifanya kiwe maarufu zaidi na kisikimbiwe na wanachama.
Yeye akiwa hana mpango wa kugombea, na hakutaka kabisa, kamati ya vijana CHADEMA wakiwemo akina Mnyika,Mdee,Kigaila na Zito na viongozi wa ngazi za juu wa chama walimshindikiza agombee nafasi ya uraisi vinginevyo wangejivua nafasi zao chamani.Hapo ndipo alipoamua kujituma ndani kinyang'anyiro hicho cha uraisi alichoambulia nafasi ya tatu nyuma ya Lipumba na Kikwete.Pia katika uchaguzi huo alikuwa na mawakala 4000 tu kati 40000 walioitajika kwahiyo huwezi kuondoa uwezekano wa kuibiwa kura. Katika uchaguzi huo ndugu Mbowe ameeleza kwamba alitumia rasilimali fedha na rasilimali vitu vya kwake binafsi.
Ubunifu ndani ya chama. "Nilitafakari sana,nivae nini katika kampeni zangu ili nionekane tofauti na wagombea wengine,nikaenda Marekani, nikapita madukani na nikaona gwanda nikasema nitavaa hizi nguo,kipindi hicho hata wazee wa CHADEMA walikuwa hawataki kuvaa kabisa gwanda''. Pamoja na hilo, pia Mbowe anadokeza namna alivyoanzisha matumizi ya Helkopta katika kampeni zake,na anasema pamoja na kujua hatashinda lakini alitumia mbinu zote hizo ili CHADEMA iingie kwenye mioyo ya Watanzania.
Uhuru wa kugombea nafasi yoyote katika chama.Mbowe amesema kila mwanachama ana haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya chama ikiwamo uenyekiti lakini kwa mbinu za kistaarabu.Akimtolea mfano Wenye,amesema unaweza kugombea nafasi ya kuwa mbunge wa CHADEMA kwenye jimbo lake lakini endapo utatumia kashfa,matusi na mbinu chafu kumchafua chama hakitakuvumilia.Pamoja na hilo alitoa onyo kwa mfano wa namna mtu mnayesafiri naye katika ziwa victoria ndani ya boti na aanze kubomoa na kuvunja mbao za boti alafu atazamwe tuu, huo utakuwa ni wendawazimu. ''Kama sasa hivi hatupo madarakani tunagombea madaraka, jee tukiingia madarakani?huu ni uchizi'' mbowe alihoji.Kwa wale wanaopima maji,amewambia wapime tuu ili waone, lakini wakiumia wasimlaumu mtu. Akaonya pia CHADEMA ni taasisi kubwa kuliko mtu yoyote.
Dhana ya udini na ukabila.(Kwa mtazamoa wangu)Akijibu hoja za uanzishwaji wa CHADEMA kwa misingi ya udini na ukabila Mbowe alitaja waasisi wa CHADEMA kwa majina na mikoa wanayotokea. Alimtaja marehemu Bob Makani kama mmoja wa waasisi wa CHADEMA, msukuma pia muisilamu. Wengine ni Brown Ngwilulupi kutoka Mbeya,Mama Mary Kabigi Mbeya (Kiongozi wa wanawake), mwenezi Edward Barongo Kagera, Shaibu...Katibu mkuu awmu ya pili n.k.
Katika kuhitimisha mwenyekiti huyo alisema, mwaka ujao utakuwa ni wakuwavuta akina mama wengi kadiri iwezekanavyo na kazi hiyo itafanywa na wanaume wa chama na wanawake waliopo ili kuondoa lawama za mambo ya viti maalumu.Lengo kubwa ni kuondoa taswira ya chama kuonekana ni cha wanaume zaidi kuliko cha jinsia zote.
MWISHO:Kesho ndugu Mbowe atakuwa katika viwanja vya shule ya msingi vya Shekilango karibu na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino ambapo anatazamiwa kuongea na wanafunzi wa chuo hicho,wakazi wa maeneo jirani na wananchi wa Mwanza kiujumla.
EmoticonEmoticon