SUAREZ ABEBA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA


Mchezaji Bora wa Mwaka, Luis Suarez akisherehekea tuzo yake ya Shirikisho ya Mashabiki wa Soka, akiwa na mkewe Sofia.
Suarez akisherehekea tuzo yake Uwanja wa Emirates.
MSHAMBULIAJI Luis Suarez ametajwa mchezaji bora wa mwaka wa tuzo ya Shirikisho la Mashabiki wa Soka jana usiku akiwapiku Leighton Baines, Christian Benteke, Juan Mata, Robin van Persie na Pablo Zabaleta kushinda tuzo hiyo iliyohusisha wapiga kura zaidi ya 500,000.Suarez alisema kuwa "Tuzo hii si yangu peke yangu, ni pamoja na wachezaji wenzangu, uongozi na benchi la Ufundi na yeyote anayehusiana na Liverpool".
Previous
Next Post »