Kwa wakati gani ule matunda ili upate faida na hayo matunda






Utaratibu uliozoeleka na watu wengi, hata kwenye hoteli za kitalii, ni kuanza kula chakula cha kawaida na mwisho kula matunda (desert). Huo siyo utaratibu sahihi, leo nitakukumbusha na kukujuza katika jambo hili muhimu la mustakabali wa maisha yako.

NJIA SAHIHI YA KULA MATUNDA
Unapaswa kula matunda kwanza kabla hujatia chakula kingine tumboni. Matunda hayaliwi baada ya mlo kama ilivyozoeleka na watu wengi. Kwa kula matunda kabla ya mlo kunawezesha matunda hayo kuingia mwilini na kufanya kazi yake ipasavyo kama vile kusafisha mfumo wa damu(detoxification) na kuupa mwili nguvu.

Mfano; ukila vipande viwili vya mkate kisha ukala na vipande viwili vya matunda, matunda yatasagika mapema kuliko mkate. Kwa kuwa vipande vya matunda vinasagika haraka vitakosa mahali pa kupitia wakati vitakapokuwa tayari kwenda kwenye utumbo, hivyo matunda nayo yatakwama hapo.

Kwa mujibu wa watafiti wetu katika masuala ya lishe, chakula kinapoingia tumboni huumuka na kuwa na asidi, matunda yaliyokwama na kukutana na vipande hivyo vya mkate pamoja na yale majimaji ya kulainishia na kusaga chakula yaliyomo tumboni (digestive juice), matokeo yake huwa ni kuharibika kwa chakula chote na kuanza kuumwa tumbo. Kwa sababu hiyo, inashauriwa tunda liliwe kabla ya kula kitu chochote. Kama utakula baada ya kula chakula, basi iwe baada ya angalau saa moja kupita.

Baadhi ya watu wanapokula tunda au kunywa juisi hupiga mbwewe au tumbo kuunguruma na hata kuuma na kujisikia kwenda chooni. Hii hutokea hasa wanapokula ndizi mbivu. Hiyo yote inatokana na kuchanganya chakula na matunda. Hali hii inaweza kuepukwa kama matunda yataliwa kwanza kabla ya chakula kingine.

Weusi unaotokea chini ya macho, kuota mvi, upara na kuwa na wasiwasi kila mara, kunaweza kuepushwa kwa kula matunda kabla ya kula kitu kingine. Kuna dhana potofu kuwa, unapokula matunda kama machungwa na ndimu, husababisha gesi tumboni lakini utafiti wa kisayansi unaonesha kuwa matunda yote yenye asidi yanapoingia tumboni huondoka asidi na kuwa ‘alikali’.

Kula tunda na nyama zake, kama vile chungwa, ni bora zaidi kuliko kunywa juisi yake kwani nyama za matunda hayo zina kambalishe (fibres) muhimu zenye faida nyingi mwilini. Unywapo juisi, kunywa taratibu kwa kujaza mdomoni ili juisi ipate nafasi ya kuchanganyikana na mate yako kabla ya kumeza.

FUNGA YA SIKU TATU

Kufunga kula kwa siku tatu huku ukitumia matunda pekee, ni njia bora ya kusafisha mfumo wa damu na kuondoa sumu mwilini. Ili kufanikisha hilo, kula matunda na kunywa juisi za matunda tu katika kipindi chote cha siku 3 na utashangaa marafiki zako watakavyoona umenawiri.

Katika kipindi hicho cha kufunga, utakuwa ukila matunda mchanganyiko na kwa muda tofauti, hupaswi kula chakula kingine zaidi ya matunda na maji. Unaweza pia ukaandaa ‘saladi’ ya matunda au mboga, ambayo inaweza kuwa nzuri zaidi.

Ukifanikiwa kutumia njia sahihi ya kula matunda, bila shaka utakuwa umegundua siri ya urembo, maisha marefu, afya njema, nguvu, kinga ya mwili, furaha na kuishi ukiwa na uzito wa kawaida siku zote.
Previous
Next Post »