Walioiba vifaa vya gari lililochukua maisha ya Paul Walker wahukumiwa


Wanaume wawili waliokuwa wakituhumiwa kwa wizi wa vifaa vya gari la muigizaji wa Fast & Furious, Paul Walker alilopata nalo ajali na kupoteza maisha wamefikishwa mahakamani na kuhumiwa , Jumatano, August 6.
Mahakama imewakuta na hatia   wanaume hao waliotajwa kwa jina la Anthony Janow na Jameson Witty na hakimu alipendekeza kuwa kila mmoja anapaswa kufungwa jela kwa muda wa miezi sita.
Muendesha mashitaka alieleza kuwa Janow na Witty waliiba sehemu ya roof ya gari hilo na vifaa vingine.
Baada ya kukamatwa, watuhumiwa hao walijitetea kuwa walichukua vifaa hivyo kwa ajili ya kumbukumbu tu na sio vinginevyo.
Paul Walker alifariki katika ajali ya gari akiwa na rafiki yake Roger Rodas, November 30 mwaka jana huko Los Angeles, eneo la Santa Clarita.
Previous
Next Post »